03 January 2013
Mgambo washauriwa kutumia ujuzi kupunguza uharifu
Na Andrew Ignas
UONGOZI wa serikali ya Wilaya ya Temeke umewaasa wahitimu wa mafunzo ya mgambo wa wilayani humo kuhakikisha wanatumia ujuzi,na elimu walionao kuiletea maendeleo Taifa katika kuzuia ongezeko la uharifu.
Akizungumza juzi wakati wa kufungua hafla maalumu ya kuwapongeza wahitimu hao wa mgambo wa awamu ya 51 wilayani humo,Mkuu wa wilaya hiyo,Katibu Tawala wa Wilaya ya Temeke Bi.Mary Shirima alisema kuwa mafunzo waliopatiwa wahitimu hao yatumike katika kuiletea maendeleo Taifa kuimarisha ulinzi madhubuti.
"Ni imani kubwa kutokana na kile ambacho mlijifunza kwa kipindi chote mtakitumia kwa ajili ya kuijenga nchi,"alisema Bi.Shirima.
Wakati huo huo,katibu tawala huyo ameahidi kufanya mazungumzo na makampuni ya ulinzi yaliyopo wilayani humo ili kuweza kutoa vipaumbele vya ajira kwa mgambo hao.
"Kubwa zaidi ambalo nawaahidi ni kuhakikisha tunasimamia ili makampuni yote ya ulinzi yanaajiri wahitimu wa mgambo ambao ndio wana mafunzo maalumu ya kukabiliana na waharifu,"alisema.
Naye mshauri wa mgambo wa wilaya hiyo, Meja Sigebena alisema kuwa mafunzo hayo yalianza rasmi Septemba 13 mwaka jana, ikiwa na jumla ya mgambo 121 lakini waliohitimu ni mgambo 65.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment