28 January 2013

Wanasiasa wanawatia hofu wafanyakazi-TUGHENa Daud Magesa,Mwanza

KATIBU Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE), Ali Kiwenge amewashukia viongozi wa kisiasa nchini akisema kuwa kauli zao zinawatia hofu
wafanyakazi na wananchi.

Alisema kauli za viongozi hao zinatishia amani ya nchi iliyopo ,hivyo akawataka Watanzania wasiwe waoga wa kusema ukweli  kwa kauli hizo za wanasiasa.

Kiwenge alitoa kauli hiyo Jijini Mwanza jana kwenye ukumbi mdogo wa Chuo cha Benki Kuu (BOT) Capri point, tawi la Mwanza,wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Alisema kai ya viongozi wa kisiasa ni kuonyesha njia tuendako na kudumisha amani na utulivu ili wananchi wafanya kazi ya maendeleo wanapokuwa na amani ambayo ndiyo silaha pekee.

“Viongozi wa kisiasa wawe wanatokana na serikali
iliyopo madarakani au nje ya serikali hiyo,wawe ni watu wa kushawishi Umma kuleta maendeleo na kutunza amani iliyopo

"Lakini si wa kutoa kauli za kututia wasiwasi na
kutujaza hofu,tukiwaa na viongozi wa kutoa kauli zisizo na mashiko wanatuogopesha sisi wafanyakazi na wananchi,” alisema.

Alidai uwajibikaji wa pamoja kwa viongozi wa kisiasa uonekane hata pale wanapokuwa bungeni kwa kufanya jambo lao kuwa moja kwa kuwa wanalipwa posho sawa,hivyo lazima kila mtu awajibike na lazima Wabunge wa CCM wabebe roho ya uvumilivu.

Alisema wanasiasa hawajatengenezwa kutoka chuo chochote hivyo ipo haja kauli zao  zikadhibitiwa  ili kuondoa hofu na wasiwasi kwa umma kwa kuwa wanafahamu fika waajiri wao ni wananchi na si watu
wanaoitakia mema nchi.

Katibu Mkuu huyo wa TUGHE aliitaka serikali kuwalipa mishahara inayolingana na majukumu yao wafanyaki wa ofisi ya CAG ikiwa ni pamoja na kuwapa vitendea kazi vya kisasa vya ukaguzi na nyenzo za usafiri.

Alidai ili ofisi hiyo ifananefane ni vema serikali ikaajiri idadi ya wafayakazi inayolingana na idadi ya majukumu ya kazi hiyo ikiwa ni pamoja na kuwalipa
motisha,nyenzo za kisasa,kama kompyuta na magari,samani na majengo.

“Wakaguzi kupewa motisha na mishahara inayolingana.Mimi ni Mkaguzi na kwenda kumkagua Mhasibu analipwa zaidi inakuwaje.Lakini pia mazingira ya kufanyia kazi CAG yawe huru na wapewe mafunzo ya uhakika ya ukaguzi kwa kupewa nyenzo za
kisasa,”alisema Kiwenge.

Alieleza kuwa hata bajeti ya ukaguzi wanayopata ofisi ya CAG ni ndogo kulingana na mahitaji baada ya kuongezeka ka maeneo ya utawala,n endapo watalipwa vizuri watachacharika kufanya kazi kwa sababu fedha hizo ni za umma na kodi zetu.

No comments:

Post a Comment