03 January 2013
Wanachama Shekilango SACCOS washauriwa kurejesha mikopo yao
Na Leah Daudi
CHAMA cha Akiba na Mikopo cha Shekilango SACCOS, jijini
Dar es Salaam, kimewataka wanachama wake kurudisha mikopo
wanayopewa kwa wakati ili kutoa fursa kwa wengine kukopa.
Ofisa Ushirika Wilaya ya Kinondoni, Bw. Ramadhani Bukuku, aliyasema hayo Dar es Salaam jana katika mkutano wa kufunga mwaka ulioandaliwa na chama hicho na kuwataka wanachama kujenga nidhamu ya kurudisha mikopo yao kwa wakati.
Alisema baadhi ya wanachama wanapotaka kukopa, wanakuwa
na kauli nzuri lakini wakishapewa, wanashindwa kuirudisha kwa
muda waliopewa hivyo kumwamisha maendeleo ya SACCOS.
“Baadhi ya viongozi na wanachama, hawatekelezi wajibu wao ipasavyo hata katika kuongoza vyama vya ushirika, hali hii inachangia kuwa na watu ambao si waaminifu katika
vikundi na kusababisha migogoro,” alisema.
Aliongeza kuwa, miongini mwa changamoto zinazojitokeza kwa baadhi ya wanachama ni kushindwa kulipa mikopo yao hivyo kulazimika kutumia akiba na hisa zao kulipia madeni kitendo ambacho kinachangia kudhoofisha vyama vya ushirika.
Alisema taarifa za baadhi ya wakopaji haziridhishi na kusababisha kuwepo migongano kati ya wakopaji na wasimamizi wa mikopo ambapo jambo hilo ni hatari sana katika SACCOS.
Bw. Bukuku alisema njia pekee ya kufanya jamii kuondokana na matatizo madogo madogo ni kujiunga katika vyama hivyo kinyume na hapo vigumu kuyafikia maendeleo.
“Nawaomba Watanzania tuache tabia ya kutegeme ajira badala
yake tujiunge kwenye vyama ya Akiba na Mikopo ili tuweze
kuinua kipato cha familia na kukuza uchumi,” alisema.
Aliwataka viongozi wanaopewa dhamana ya kuendesha SACCOS hizo, kuacha tabia ya kuegemea upande mmoja na kuangalia sura
ya mtu kwani kwa kufanya hivyo vyama vitakosa maendeleo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment