04 January 2013

TMA YAHADHARISHA WANANCHI MVUA ZINAZONYESHA NCHINI

Na Grace Ndossa

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania(TMA)imewataka wananchi waendelee kuchukua tahadhari kutokana na mvu zinazoendelea kunyesha ambazo ziko nje ya msimu.


Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana na Mkurugenzi wa mamlaka hiyo Dkt Agnes Kijazi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tathimini na mwekeleo wa mvua nchini kwa kipindi cha Januari hadi machi mwaka huu.

Alisema kuwa ni vyema wananchi wakachukua tahadhari  kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha zinaweza kusababisha maafa kwa wananchi .

Pia alisema kuwa maji yanatakiwa yatumiwe kwa uangalifu hasa shughuli za umwagiliaji katika maeneo ya mito inayotiririsha maji kwenye mabwawa ya kuzalisha umeme ili kuwa na uhakika wa kupata maji ya kutosha katika mabwawa.


"Katika kipindi cha  mvua kilichobaki ni kifupi hivyo pamoja na matarajio ya mvua za wastani hadi juu ya wastani katika baadhi ya maeneo ya kati na kusini mwa nchi tunashauri maji yatumike kwa uangalifu hasa shughuli za umwagiliaji katika mito inayotiririsha maji kwenye mabwawa ya kuzalisha umeme,"Alisema Dkt Kijazi.


Alisema kuwa kuna uwezekavyo wa kuwa na vipindi vifupi vya mvua kubwa zinazoambatana na upepo mkali katika kipindi hichi ch mvua hivyo tahadhari ziendelee kuchukuliwa ili kuhakikisha usalama  wa wananchi na mali zao.


Hata hivyo alisema kuwa mwezi huu mvua zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani, isipokuwa maeneo ya kaskazini magharibi ambayo yanayotarajiwa kuwa na mvua za wastani hadi chini ya wastani.


Alisema kuwa  kutokana na mabadiliko y hali ya hewa viwango vya mvua ya wastani vinaendelea kushuka hivyo kufanya mvua za wastani katika baadhi ya maeneo kutokidhi mahitaji ya shughuli mbali bali za kilimo maji na nishati.

Akizungumzia  mifumo ya hali ya hewa iliyokuwepo katika kipindi cha oktoba  hadi Disemba 2012 hali ya joto la bahari  katika ukanda wa tropiki ya mashariki mwa bahari ya  Pasifiki iliendelea kushuka kutoka juu ya wastani hadi wastani.

Alisema kuwepo kwa joto la juu ya wastani katikati mwa bahari ya Hindi na pwani ya Somalia na mgandamizo mkubwa wa kusini mashariki mwa pwani ya Tanzania kulisababisha kupungua  kuvuma kwa upepo wenye unyevuunyevu.

Aidha kutokana na mabadiliko  hayo yasiyokuwa ya kawaida  taasisi zinazohusika na masulaya  hali ya hewa katika kanda ya pembe ya Afrika(ICPAC),na kanda ya kusini mwa Afrika(SADC-CSC)ilikutana na wataalmu na kufanya uchambuzi wa mifumo ya hali ya hewa na kutoa mrejeo wa mwelekeo wa mvua za msimu.

Alisema kuwa  wal;ibaini kuwa chanzo cha kuchelewa kunaza kwa msimu wa mvua ilisababishwa na kutokea kwa kimbunga kiitwacho ANAIS mwanzoni mwa oktoba 28 2012 katika eneo la kusini magharibi mwa bahari ya hindi ambacho kilisababisha mwelekeo wa upepo wenye unyevu unyevu kuvuma kuelekea katikati ya bahari ya hindi

Vile vile kilitokea kimbunga kingine MURJAN katikati ya oktoba 2012 katika pembe ya afrika ambacho kilisababisha mfumo wa mvua kubaki kaskazini mwa ikweta hali iyosababisha  kupungua kwa mvua.

No comments:

Post a Comment