03 January 2013
TAKUKURU Moro yatoa akizo kwa madereva
Na Severin Blasio, Morogoro
MKUU wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), mkoani Morogoro, Bi. Stella Mpanji, ametoa
wito kwa wananchi hasa madereva kutoa taarifa wanapoombwa
rushwa na baadhi ya wafanyakazi wasiowadilifu wa mizani za Mikese, Kihonda na Mkumi ili waweze kuchukuliwa hatua.
Bi. Mpanju alitoa wito huo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya taasisi hiyo kuwakamata wafanyakazi watatu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS).
Wafanyakazi hao walikamatwa Desemba 10 mwaka huu ambapo Desemba 13 walifikishwa katika Mahakamani ya Wilaya ya Morogoro.
Aliwataka washtakiwa hao kuwa ni Bi. Happiness Minja (29), Bw. Victor Mongi (30) na Bw. Eliud Mwakamela (29), ambao wote ni wafanyakazi katika Kituo cha Mizani Mikese mkoani humo.
Alisema siku ya tukio, Bi. Minja aliomba rushwa ya sh. 40,000 kutoka kwa dereva w lori lililokuwa limezidisha uzito na baada
ya kupewa fedha hizo, aligawana na wenzake wawili ambao
pia ni washitakiwa katika kesi hiyo.
Aliongeza kuwa, washtatiwa wote wanakabiliwa na kosa la kuvunja sheria ya kuomba na kupokea rushwa kifungu cha 15(10)(a) namba 11 ya mwaka 2007.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment