18 January 2013

Shibuda achoshwa na vitisho Chadema *Sasa kuanika siri ya mgogoro unaondelea kufukuta *Adai chama hicho hakina mvuto tena Kanda ya ZiwaNa Benedict Kaguo

MBUNGE wa Maswa Magharibi, mkoani Simiyu, Bw. John Shibuda (CHADEMA), anakusudia kuuweka wazi mgogoro unaondelea ndani ya Chama hicho.


Alisema kama chama hicho kitaendelea na mfumo unaotumika sasa, upo uwezekano wa kufia mikononi mwa Mwenyekiti wake Taifa, Bw. Freeman Mbowe.

Bw. Shibuda aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na gazeti hili juu ya tuhuma zinazotolewa dhidi
yake kukichafua chama hicho na taarifa za kuwepo uwezekano
wa kufukuzwa uanachama.

Alisema dhamira yake ni kukutana na viongozi wakuu wa chama hicho Bw. Mbowe na Katibu Mkuu Dkt. Willibrod Slaa ili aweze kuwauliza kinachoendelea ndani ya chama hicho.

Aliongeza kuwa, amechoshwa na taarifa za vitisho vya kufukuzwa ndani ya chama hicho na kudai kilichomuondoa CCM ni kupinga dhuluma na ugandamizaji.

“Wakati nikihamia CHADEMA, niliamini chama hiki kina demokrasia makini jambo ambalo ni tofauti na ilivyo sasa.

“Siwezi kila siku kutishiwa kufukuzwa na watu ambao ni mgodi wa uhalifu wa kutumia vibaya madaraka na kufinya uhuru wa wengine kutoa maoni, sikubaliani na maovu ya chama chochote cha siasa,” alisema Bw. Shibuda.

Aliongeza kuwa, kutokana na machafuko yanayoendelea katika vyama mbalimbali vya siasa nchini, anaunga mkono hoja ya kuwepo mgombea binafsi ambayo ndio itakuwa dawa ya kuondoa dhuluma iliyojaa kwenye vyama vya siasa.

Bw. Shibuda alisema, wananchi wa Kanda ya Ziwa wamemtaka awaeleze ubora wa CHADEMA kwa masilahi ya Taifa siku zijazo kwani taswira waliyonayo, chama hicho kina uongozi wa kimila
na kufukuzana badala ya kufundishana.

Alisema chama hicho kimepoteza kura za wananchi wa kanda hiyo katika Uchaguzi Mkuu ujao ambao hawana mvutoa nacho tena.

“Niko tayari kwa mdahalo kuelezea hili, msimamo wa Kanda ya Ziwa hawatakubali kuitwa kubwa jinga kwa kubeba watu kuingia madarakani,” alisema.

Aliongeza kuwa, ujuzi na uzoefu alionao katika siasa haufanani na kiongozi yoyote ndani ya CHADEMA kwani alianzia kuwa mjumbe wa nyumba kumi hadi kufikia mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC).

31 comments:

 1. WEWE SHIBUDA TULISHAKUJUA,CCM ULIHAMA HIVI HIVI, ULITAKA URAISI WAKAKUNYIMA, SASA TENA UNATAKA KUCHAFUA TENA CHAMA HIKI, TUNAOMBA UUNDE CHA KWAKO UONE KAMA UTAPATA URAISI,MIMI NAAMINI HUWEZI MAANA WE MNAFIKI, MTU AMBAYE UNAPENDA MADARAKA, SIO MAENDELEO.UNAJUA BWANA SHIBUDA KAMA HUNA HOJA YA MSINGI BRO USIONGEE, MIMI NAAMINI 2015 HAUTAPATA UBUNGE KAMA HALI YAKO NDIYO HIYO.EBU KUWA NA MSIMAMO.WAKATI UNATOKA CCM ULIKUWA UNASEMA CCM WABAYA SABABU WALIKUNYIMA URAISI YAANI UNATAKA WATU WAKUSIKILIZE WEWE.ACHA HIVYO.TUNAUMIA SANA KILA CHAMA UKIJIUNGA UNAVURAGA. WE MWANA CCM ULIYETUMTUMA KWENDA KUHARIBU VYAMA.ACHA MAMBO YA AJABU

  ReplyDelete
  Replies
  1. SHIBUDA HANA UBABE MBABE NI SLAA NA HENJE WANAUA CHAMA

   Delete
 2. BORA URUDI CCM KUNA DEMOKRASIA YA KWELI UNAYOITAKA IACHE CHADEMA TUNARIDHISHWA NA DEMOKRASIA ILIYOKO CHADEMA WEWE RUDI CCM UTAGOMBEA URAIS. KWA CHADEMA HUTOIPATA HATA UVUE NGUO.CHADEMA MPO JUU ACHANENI NA HAO WENYE NIA MBAYA NA HIKI CHAMA CHA UKOMBOZI WA NCHI HII KWA AWAMU YA PILI.CCM WAMETUNYIMA MKOPO TULOMALIZA KIDATO CHA SITA MWAKA 2007 KISA TUMESOMEA ARTS ILA SAYANSI HATA 2000 WAMEPEWA TUNATESEKA VYUONI KAMA WAJANE WASOKUWA NA WAZAZI.HUKU NI KUTUGAWA WATANZANIA.ARTS NA SAYANSI TOFAUTI IPO WAPI?KIKWETE NA KAWAMBWA TUFIKIRIE TUPATE HATA ADA TU HAPA UDSM NA TUNASOMEA UALIMU KWA NINI SAYANSI WAPATE MKOPO SISI TUKOSE?.MUNGU IBARIKI TANZANA.AMEN

  ReplyDelete
  Replies
  1. SHIBUDA NAKUSHAURI UBABE HAUNA NAFASI TENA,UMRI WAKO NI HESHIMA KUANDAA VIJANA KAMA JOSHUA,MNYIKA,MDEE,MBILINYI NK WAKOMAE KISIASA WE UNAJISIFU UNAJUA MPAKA LINI UTAKUBALI WENZAKO LINI? YAMKINI UNATUMIKA NA IMANI YETU IANPUNGUA KWAKO. NAKUOMBA JENGA HISTORIA NZURI YA MAISHA YAKO NA VIZAZI VIJAVYO KISIASA.

   Delete
  2. SHIBUDA NAKUSHAURI UBABE HAUNA NAFASI TENA,UMRI WAKO NI HESHIMA KUANDAA VIJANA KAMA JOSHUA,MNYIKA,MDEE,MBILINYI NK WAKOMAE KISIASA WE UNAJISIFU UNAJUA MPAKA LINI UTAKUBALI WENZAKO LINI? YAMKINI UNATUMIKA NA IMANI YETU IANPUNGUA KWAKO. NAKUOMBA JENGA HISTORIA NZURI YA MAISHA YAKO NA VIZAZI VIJAVYO KISIASA.

   Delete
  3. SHIBUDA NAKUSHAURI UBABE HAUNA NAFASI TENA,UMRI WAKO NI HESHIMA KUANDAA VIJANA KAMA JOSHUA,MNYIKA,MDEE,MBILINYI NK WAKOMAE KISIASA WE UNAJISIFU UNAJUA MPAKA LINI UTAKUBALI WENZAKO LINI? YAMKINI UNATUMIKA NA IMANI YETU IANPUNGUA KWAKO. NAKUOMBA JENGA HISTORIA NZURI YA MAISHA YAKO NA VIZAZI VIJAVYO KISIASA.

   Delete
  4. Kijana andamana, goma upate ada.Ni haki yako. Achana na siasa za vyama.Hakuna shetani mzuri duniani. Wamalawi walisababisa rais wao akafa kwa msongo alipokua akijitahidi watu wake wafanye kazi wajitegemee. Wakashangilia kifo chake. Leo wapo barabarani wanaaandamnana. Wewemwana art mzuri soma historia hata ya hivi punde

   Delete
  5. Sema umefeli wewe, wenzako kibao wamesoma arts na wanamkopo. Na wengine wengi watafuata, sema jingine sio hilo. Unapotosha ukweli.

   Tena hustahili hata kujiita msomi.SIASA ni kazi. Always think postive for your own future and for others. tanzania is good and we must all build her regardless our ideologies. CCM ni chama na CHADEMA ni chama, Shibuda ni mwananchi mwenzetu, kwanini akisema yeye awe mbaya isipokuwa Mbowe na Slaa? Tutafute ukweli ndugu yangu.

   Nakutakia kila la kheri na Mungu akufanikishe katika masomo yako.

   Delete
 3. SHIBUDA WE NI KIMELEA CHA CCM.HUNA DIRA NA USIFIKIRI KANDA YA ZIWA INAKUSIKILIZA WEWE.YAANI TUKO MBELE NA KAMWE HUWEZI KUICHAFUA CHADEMA BADALA YAKE UNAJICHAFUA MWENYEWE.KAMA UMETUMWA NA CCM WAAMBIE IMESHINDIKANA ACHA KUJISHUSHIA HADHI UZEENI.

  ReplyDelete
 4. KAMA ULIANZIA UBALOZI WA NYUMBA KUMI MPAKA UNNEC KILICHOKUONDOA CCM NA KUJA CHADEMA NINI?UNAPOTEZA MUDA WAKO KANDA YA ZIWA BADO TUPO NA CHADEMA UMEBAKI PEKEYAKO

  ReplyDelete
  Replies
  1. HAYO NI MAKOSA CCM WALIFANYA SIDHANI WATAYARUDIA NDIO SABABU BAADHI YA VIONGOZI WA CCM WALILAZIMISHWA KUSTAAFU,PILI CCM IMEACHA KUIMBA WIMBO WA CHADEMA SI RAHISI TENA CHADEMA KUFURUKUTA WALIZOEA KULA MATAPISHI YA CCM KAMA MBWA WATAKUFA NJAA HAYAKUWEPO NI SAWA NA FISI ANAYETEMBEA NYUMA YA BINADAMU AKITEGEMEA MIKONO YA BINADAMU ITANG'OFOKA ALE SINA UHAKIKA

   Delete
 5. Shibuda,ulikutana lini na wanakanda ya Ziwa hata wakakutuma uwasemee kuwa CHADEMA imepoteza kura zake kwao uchaguzi ujao 2015?!Mbona unapenda kujipa umaarufu usio wako bwana?? Naamini wanakanda ya Ziwa si wajinga kamaunavyotaka ionekane,mimi ni mwanakanda hiyo lakini sijakutana na wewe na kukutuma!!Pia nimejaribu kuuliza wanzangu kadhaa kujua labda ulikutana nao kisha wakakutuma,wote wamekana sasa wewe utaarishi huo umepewa na nani?Acha hizo bwana mkubwa wewe sasa.

  ReplyDelete
 6. KWELI KIJANA WA MKOPO MIMI NIPO CHUO HAPA IRINGA NASOMEA UALIMU KAMA WEWE NIMEKOSA MKOPO PIA KISA NIMESOMA ARTS NA NIMEMALIZA FORM SIX 2010 KURUDI NYUMA RAIS WETU MPENZI KIKWETE TUFIKIRIE HATA KIDOGO YA ADA TU TUNATESEKA.HADI TUMEANZISHA CHAMA CHA WALIOKOSA MKOPO ILI TUSAIDIANE ILA MAMBO BADO MAGUMU RAIS WETU NA INAUMA KWA NINI SAYANSI HAWANA HIVYO VIGEZO SISI ARTS TUNABANWA NA HATUKUPENDA TUWE ARTS NI MAZINGIRA TU TUNAOMBA HATA ADA PAMOJA NA KUAPPEAL TUNAONA UKIMYA.NA INAUMA TUNAPOONA NCHI IPO TULIVU NA WENGINE TUNAPANGA KUANDAMANA KUDAI HIYO HAKI KAMA WATANZANIA WENGINE.MASKINI KAMA SISI.TUNAOMBA SERIKALI ITUSAIDIE HATA ADA TU MILIONI MOJA.KWA MWAKA.MUNGU IBARIKI TANZANIA

  ReplyDelete
  Replies
  1. HAMIENI CHADEMA MIKOPO IKO NJE NJE

   Delete
 7. Sidhani kama shibuda alifikiri vizuri kabla ya kutoa msimamo wa wanakanda ya ziwa. Shibuda ni nani, amefanya nini cha maana hapa Tanzania zaidi ya kugonga meza na kukubali hoja zinazowaumiza watanzania kila kukicha wakati akiwa kwa magamba, wala hakuhama CCM kwa kuchoshwa na ukiritimba na uzandiki wa CCM bali ni kwa sababu alikosa nafasi. Hebu tupishe Shibuda usifikiri watanzania bado ni wajinga tunajua baya na jema wala huna haja ya kutufundisha.

  ReplyDelete
  Replies
  1. SHIBUDA ANAYEPENDWA KWENYE JIMBO LAKO NI WEWE WALA SIO CHADEMA HATA MGOMBEA BINAFSI WA JIMBO HILO UTAPATA ILA CHADEMA WAMECHIMBA KABURI WAKO NDANI NI UDONGO TU HAUJAFUKIWA KAMA NI UONGO WAJARIBU KUFANYA UCHAGUZI IWAPO MADIKTETA HAWATAPIGWA CHINI WOTE

   Delete
 8. Shiba wewe ni mfa maji kutapatapa lazima. sisi ndio tuko kanda ya ziwa na wala si kanda ya Shibuda CHADEMA tuko tele. Mkakati ni kukuondoa kwenye ubunge kwani hata cc wananchi ushatuchosha kwa mafumbo na vijembe vyako bungeni matatizo na kero za wananchi haujazitatua bado. Rudi ccm huku mbwembwe hazina nafasi CHADEMA kaazi tu.
  MUNGU IBARIKI CHADEMA MUNGU IBARIKI TANZANIA.

  ReplyDelete
 9. SHIBUDA KOKOTE UTAKAKOELEKEA WAPIGA KURA WAKO WANAKUTATA WEWE SIO CHAMA ILA ULIHABIA CHAMA HICHO BILA KUFANYA UTAFITI WAKO WALIOSEMA BAVICHA NI BAA YA VICHAA a.k.a BAA YA WEHU JARIBU KUWAOMBEA WATOKE PEPO LA UKICHAA

  ReplyDelete
 10. ACHA MAMBO YAKO WE SHIBUDA KAMA VP RUDI KWA WALIOKUTUMA KAWAMBIE NIMEKOSA MLANGO WA KUINGILIA CHADEMA HAPAINGILIKI FISADI TU

  ReplyDelete
 11. NA NYIE MAJIRA HAMNA STORY NYINGINE ZA KUANDIKA? KILA SIKU PICHA YA KIKWETE STORY YA CHADEMA, MBONA HAMCHANGANYI STORY, NASHANGAA LEO MMEWEKA KUWA WANANACHA WA CHADEMA WAMKANA SHIBUDA KUWA CHAMA KIMEPOTEZA MVUTAO. BADILIKENI. MUWE KAMA GAZETI HURU KWELI, MAANA HUYO MWANDISHI WENU KAGUO ANALETA STORY BILA KUWA NA URARI-KUBALANCE. MSISHABIKIE SIASA SANA.


  MAANA KUHU MITAANI TUNAAMBIWA KUWA HALI YENU NI NGUMU PIA, HAMLIPI WAFANYAKAZI KWA MWAKA SASA NDIO MAANA WAKIPATA MDAU WA KUWALIPA LAZIMA WALETE STORY MBAYA.

  KWA HILO PIA JITAHIDII JAMANI, MAISHA NI MAGUMU SANA, MNAPOWANYIMA WAFANYAKAZI WENU HAKI ZA MSINGI HAMUWATENDEI HAKI, WAO WANAOUMIA ILA MUNGA ANAJUA ADHABU YENU.

  ReplyDelete
  Replies
  1. NDUGU GAZETI LA MAJIRA, MTANZANIA NA JAMBO LEO YAMENUNULIWA NA MAFISADI WA CCM, NDIO MAANA SOKONI YAMEDOLOLA HAKUNA WA KUYANUNUA! SHIBUDA NAMSHAURI AACHANE NA SIASA KWA KUWA WATANZANIA TUMEMCHOKA, TENA AACHE KUTUTUMIA SISI KANDA YA ZIWA KAMA KINGA YAKE KWA KUWA SISI NA CHADEMA NI DAMU DAMU

   Delete
 12. kushiney CHADEMA, kwisha habari yenu

  ReplyDelete
 13. shibuda sio kanda ya ziwa, kama unaamini unaonewa hama chadema, vyama ni vingi nenda SAU, au ADC nk kule bado wamelala utapata, chadema waachie wenyewe, wewe sio kanda ya ziwa au ndo unataka kuleta chama cha kanda ya ziwa.

  ReplyDelete
 14. CCM wamezeeka kiasi wanajikojolea hovyo na hao CHADEMA wehu kabisa. wananchi wamepata mshangao

  ReplyDelete
 15. CCM THINKS OF KILLING CHADEMA LET THEM KNOW THAT TODAY IS NOT WHEN THEY MANAGED TO STRANGLE NCCR AND CUF USING PUBLIC RESOURCES. YOU HAVE FAILED USING POLICE AND EVEN USALAMA WA MASISADI YOU EMPLOYE IS DOOMED TO FAILURE. TANZANIA NEEDS CHANGE BAD OR GOOD. 50 YEARS OF UHURU WE ARE UNABLE EVEN TO ERADICATE MOSQUITOES EXPECTING THE USA TO DO FOR US!

  ReplyDelete
 16. EBwanaeee, kumbe ndiyo mambo yalivyo ndani ya Chadema? Eleweni Chadema ni Mtei = Bob Mkwewe + Mbowe Mkwewe sasa mnategemea nini? ilianza kama Saccos sasa eti ni Chama na kura zitoke Kanda ya Ziwa. Hivi huko Mwanza na Shinyanga Kagera na Musoma ndiko waliko Mabwege? wanataka daraja la kupandia? labda waende Kg maanake huko ni kama Wakimbizi ubishi umewajaa. Shibuda anasema ukweli na ukweli siku zote unauma.Hongera sana Shibuda hupepesi wala kuuma maneno umewamwagia Mwaaaaaaa

  ReplyDelete
 17. GAZETI LA MAJIRA NAOMBA MCHANGIE CHADEMA ANGALAU 20% YA MAPATO YENU,KWANI HABARI ZA KUPIKA ZA CHADEMA ZIMEWASAIDIA SANA KUUZA MAGAZETI YENU.KUWENI WAAMINIFU JAMANI.ASANTENI

  ReplyDelete
 18. shibuda anataka umaarufu tu.

  ReplyDelete
 19. chadema mfukuzeni shibuda kama cuf walivyo mfukuza hamadi rashidi wanavuluga vyama vya upinzani.

  ReplyDelete
 20. Chadema mnamchelewesha huyu msaliti mfukuzeni kabla ajawaletea madhara. Huyo Shibuda ni nyoka tu.

  ReplyDelete
 21. shibuda acha wizi wako ni mambo ya ajabu sana kawaulize wana political science watakuambia unakaa upande gani huo ni ujinga sana kaka shibuda acha ujinga bhana

  ReplyDelete