04 January 2013
SAKATA LA GESI MTWARA Muhongo sasa achafua hewa *CUF wadai hana hoja, amekurupuka *Zitto asema serikali imeshikwa tamaa
Rehema Maigala na Rehema Mohamed
KAULI ya Waziri na Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, kudai gesi ya Mtwara lazima isafirishwe kwenda Dar es Salaam kutokana na faida za mradi huo kwa Taifa, imeonekana kuchafua hali ya hewa baada ya wadau mbalimbali kuipinga.
Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti, wadau hao walidai Prof. Muhongo amekurupuka kwa majibu aliyotoa bila kutafakari kwa kina madai ya wananchi ambayo ni ya msingi.
Askofu wa African Inland Church, Charles Salala, alitetea msimamo wa wananchi mkoani Mtwara na kudai maandamano waliyofanya ni ya msingi ili kudai miundombinu ya gesi ijengwe mkoani humo na kutumike kwa kuharakisha maendeleo ya sekta mbalimbali.
“Maandamano ya wakazi wa Mkoa huu yalikuwa sahihi kwani walikuwa wanatimiza matakwa ya Katiba ya nchi, majibu ya Prof. Muhongo hayaoneshi kama alifanya utafiti, kama mindombinu ya
gesi itajengwa Mtwara, itapunguza msongamano wa watu kukimbilia Dar es Salaam ili kutafuta kazi,” alisema.
Kwa upande wake, Chama cha Wananchi (CUF), kimedai kushangazwa na tamko la Serikali alilolitoa Prof. Muhongo.
Akizungumza na gazeti hili, Naibu Mkurugenzi wa Habari na Mahusiano ya Umma wa CUF, Bw. Abdul Kambaya, alisema chama hicho kinahoji kwanini Kiwanda cha Makaa ya Mawe hakijajengwa Dar es Salaam wala usafishaji dhahabu badala
yake unafanyika katika maeneo ya uchimbaji.
“Wakazi wa Mtwara wanaendeleza utaratibu ule ule ulioasisiwa
na Serikali wa kuacha dhahabu iliogunduliwa katika maeneo ya Mwanza, Arusha, Mara, Geita, Shinyanga, Manyara na Makaa ya Mawe pale Mbeya, yaendelee kuchimbwa na kusafishwa kwenye maeneo hayo ili kuongeza ajira kwa wakazi wa maeneo husika,” alisema Bw. Kambaya.
Aliongeza kuwa, hoja ya watu wa Mtwara si kuzuia mapato yatokanayo na gesi bali ni kujengewa viwanda ambavyo
vitatumia malighafi ya gesi ili kuongeza ajira.
Alisema hoja ya Watanzania wote kunufaika na mapato yatokanayo na maliasili ni sahihi na wakazi wa Mtwara hawaweze kuipinga kwani mapato yatatokana na viwanda ambavyo vitajengwa mkoani humo pia yataingia kwenye pato la Taifa.
Bw. Kambaya alisema hata kampuni iliyopewa tenda ya kutengeneza bomba la kusafirisha gesi hiyo kutoka Mtwara hadi
Dar es Salaam, ilitoa ushauri kwa Serikali kujenga Kiwanda cha Mbolea mkoani humo ili kuongeza ajira kwa vijana lakini haujazingatiwa.
Chama cha NCCR-Mageuzi, kilisema Serikali inapaswa kuwasikiliza wananchi badala ya kuwabeza. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Saalam jana, Mwenyekiti wa chama
hicho Bw. James Mbatia, alisema wananchi wa Mtwara wana haki yao, hivyo Serikali ikae nao mezani ili kutafakari hoja zao.
Alisema Serikali isirudie makosa waliyofanya katika miradi iliyopita kama ya uchimbaji madini ya dhahabu, almasi na makaa ya mawe ambayo wananchi wa maeneo husika hawanufaiki kwa lolote.
“Tunatoana ngeu kwa sababu ya gesi, haya yote yasingetokea kama tungeshirikishwa, mtu anauliza atanufaika vipi na rasilimali yake unamuita muhuni, tusiwabeze wana Mtwara,” alisema.
Bw. Mbatia alidai kuishangaa Serikali inaposema maandamano yaliyofanywa na wananchi yaliratibiwa na wapinzani wakati kulikuwa na baadhi ya viongozi wa CCM katika Mkoa huo.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zitto Kabwe (CHADEMA), alisema kauli ya Serikali ni kielelezo kuwa haihitaji kabisa kujua uhuru wa watu wa Mtwara na Lindi, licha ya kuwa wachangiaji wakubwa katika uchumi wa Taifa kupitia zao la Korosho.
Alisema Serikali inataka kufuta historia ya mchango wa zao la Korosho kwenye uchumi wa nchi kwa tamaa gesi asilia.
“Wakati Jiji la Dar es Salaam linapiga hatua ya maendeleo, mikoa
ya Lindi na Mtwara inawalinda wakazi wa jiji hilo na mikoa mingine waendelee kuishi kwa amani na starehe, Serikali inapimaje mchango wa mikoa hii...tunaipima kwa fedha? alihoji Bw. Kabwe.
“Serikali inasema lazima bomba la gezi lije Dar es Salaam kwa sababu jiji hilo ndio linalozalisha asilimia 80 ya mapato ya Serikali, huu ni uongo na aibu kubwa kwa Serikali,” alisema.
Aliitaka Serikali itoe orodha ya walipa kodi wakubwa 100 ili kuona uzalishaji halisi wa mapato hayo unafanyika wapi.
Naye Mbunge wa Vunjo, mkoani Kilimanjaro, Bw. Agustino Mrema, alisema maandamano ya wananchi mkoani Mtwara ni matokeo ya kuonekana wasindikizaji wa maendeleo.
Alisema watu wa Kilimanjaro wakiona wenzeo wa Mtwara wamefanikiwa katika madai yao na wao watafanya maandamamno ya kudai rasilimali zilizopo mkoani humo ili ziwanufaishe.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
KWA HIYO NA KIKWETE HOTUBA YAKE HAINA MAANA MBONA AMEWAPUUZA WANAPINGA GESI KUELEKEA DAR WALA WAZIRI WA NISHATI ANATEKELEZA SERA ZILIZORIDHIWA NA CCM WOTE WANAHUBIRI TOFAUTI NI WANAFIKI NI BORA WAITWE NA KUONYWA WANAVURUGA SERIKALI
ReplyDeleteMBONA JAMBO HILI LINAKUA MATAJI WA KISIASA? WANANCHI WAELIMISHWE VIZURI ZAIDI KWA JINSI WATAKAVYOFAIDIKA NA UVUMBUZI WA GESI. WANASIASA HAWA NI WASOMI. WAO WANELEWA VIZURI SANA NGOMA WANAYOCHEZA. MAELEZO YAO SIO YA KTAALAMU. WANAFAHAMU UTASHI WA KUAMUA ENEO LA KUJENGE KIWANDAKAMA GHARAMA ZA USAFIRISHAJI, UZITO WA BIDHAA NA SOKO. RAIS NA WAZIRI WAKE WAMEPATA USHAURI WOTE WA KITAALAMU KUTOKA NJE NA NDANI YA NCHI. HAWAJAKURUPUKA!
ReplyDeleteTUMECHOKA KUSINDIKIZA MAENDELEO, KWANI MAENDELEO DAR TU, MBONA HATUKUSIKIA GESI IPELEKWE SINGIDA IKALETE MAENDRELEO, SERIKALI INAICHUKIA MIKOA YA KUSINI NDO MAANA TUPO NYUMA KIAMENDELEO, KAMA BARABARA YA KM 60 INA MIAKA ZAIDI YA 8 HAIJAISHA LEO VP GESI IPELEKWE DAR, KAMA DGRIDI YA TAIFA HAIJAFIKA MTWARA MPAKA TULIPOPATA GESI 2004 NDIPO UHAKIKA WA UMEE LEO VIPI KILA KITU DAR, SERIKALI WALISHALIGAWA TAIFA ZAMANI KATIKA HAYA MAKUNDI YA KIMAENDELEO KWA HIYO WANACHOFANYA MTWARA NI KUWAONESHA DHAMBI YAO NA HILO NDILO LINALOWAUMA KWA KUWA NI KWELI, VIPI UACHE BANDARI YA MTWARA, LINDI, TANGA ZIKIWA HAZINA KAZI KWA KUTOKURABATIWA NA KUWEKEWA MAZINGIRA MAZURI YA KUTUMIKA UAKCHIMBE BANDARI BAGAMOYO? HUU NI UBAGUZI NA LAZIMA UWAUMIZE
ReplyDeleteTUANGALIE SANA NA KAULI ZETU KAMA INAFIKIA HATUA ZIKO NCHI ZINADAI ZIFIDIWE NA MATAIFA YALIYOENDESHA UKOLONI AFRIKA KAULI ZA TANZANIA ZIKIKUTANA NA WATU WASIO NA HEKIMA NA BUSARA HII NCHI SI UONGO ITAMEGUKA VIPANDE VIPANDE SINA UHAKIKA KAULI HII INAELEWEKA IKO MIKOA ILIYOKUWA IKIZALISHA MKONGE ,PAMBA,KAHAWA NA TUMBAKU AMBAYO YALILIINGIZIA TAIFA FEDHA ZILIZOTUMIKA KWA TAIFA ZIMA MPAKA ARDHI IMEHARIBIKA JE WAKTAKA WALIPWE FIDIA MIKOA ILIYOFAIDIKA INAWEZA KUFIDIA ?? IRINGA [ISIMANI]IKIONGOZA KWA KUZALISHA MAHINDI 1972 JE KUNA KINU CHA KUSAGA SEMBE PALE HIVI NI NANI HAWA WAKOLONI MAMBOLEO?? HIVI MUNAJUA ALIMAS YA MWADUI ILIVUMBULIWA LINI KAMASI 1940 MBONA KIWANDA CHA KUKATA ALIMAS KILIKUWA IRINGA MUNATAKA KUSEMA WASUKUMA WA MWADUI WAO WALIKUWA MAZUZU,JE TUMBAKU KULIMWA TABORA KUNA KIWANDA CHA SIGARA PALE ?? YATATOKEA MADAI YA FIDIA KWA UHARIBIFU WA MAZINGIRA KWENYE MAENEO AMBAYO RASILIMALI ZIMEVUNWA ZIKATUMIKA KWA FAIDA YA TAIFA ZIMA HIVI LIPUMBA AKIAMBIWA TUMBAKU TULIYOLIMA TABORA TUKAKATA MITI YOTE TABORA NI JANGWA MBONA FEDHA ZA TUMBAKU HAZIKUONEKANA KWENYE NYUSO NA MIILI YETU HIVI MREMA WACHAGA WAKIDAI FIDIA KWA KAHAWA ILIYOUZWA NA FEDHA KUTUMIKA KWA MAENDELEO YA TANZANIA NZIMA MPAKA ARDHI IMECHOKA MUKO TAYARI KUFIDIA UHARIBIFU WA ARDHI YA WACHAGGA ,WASUKUMA NAO WATATAKA PAMBA YAO ILIYOTUMIKA KUVALISHA NGUO WATANZANIA WOTE MPAKA ARDHI IKAHARIBIKA WAFIDIWE HARAKA MJADALA HUU UNAWEZA KUIVURUGA TANZANIA ALIYETABIRI KUWA TANZANIA ITAVUNJIKA VIPANDE VIPANDE HAJAKOSEA UVUNAJI MADINI MAENEO MENGI UMEANZA KARIBUNI NA HUAMBATANA NA UHARIBIFU NANI AFIDIE TUSIJIDAI KUZUNGUMZA KWA JAZIBA BUSARA NA HEKIMA TU UNAELEWEKA WAPO WATU WENGI WEMBAMBA WANAZUNGUMZA KWA SAUTI NENE NA WENGINE WATUPA MIKONO NA MIGUU MUTAZEEKA UPESI HAKUNA HAJA YA KUZUNGUMZA MPAKA UTOE JASHO MBONA HAKUNA ZUZU
ReplyDeleteAsante sana mtoa maoni. Lakini umesahau kutaja waalaimu na wafanyakazi wengine waliolazimishwa kwenda ktumika katika mikoa ya Mtwara na Lindi katika jitihada ya kuindeleza wakapotenza maisha yao kwa kuliwa na wanyama au kwa malaria.Leo gesi tu inawasimamisha masikio. Je sisi tuliopokea majeneza ya ndugu zetu waliofanya kazi huko tuseme nini. Mungu ibariki Tanzania
DeleteMuhimu ni kwamba wanamtwara wameliona hili na kwa mtazamo wao litakuwa na athari. Kwani Usindikaji wa gesi ukifanyika mtwara kuna hatari gani, pato la taifa si litapatikana na fursa nyingi za ajira na maendeleo ya kiuchumi yataongezeka mtwara. Tuipe fursa mikoa na sehemu zingine za tanzania kukua kiuchumi, siyo kukariri kila kitu Daresalaam. Tuache ufinyu wa fikra
Deleteupinzani huu una sura mbili:nzuri na mbaya='amoral'
ReplyDeleteUkiangalia nigeria inatia kichefuchefu kuona mahali mafuta yatokako hakuna maendeleo, kwa upande wa pili wa shilingi tukiangalia maeneo ya watu watokako basi yatatushinda, tuseme wa kunufaika na dar es salaam wawe wenyeji wazaramo na mliobaki wote mrudi kwenu. Kule morogoro kuna vyuo vikuu waluguru wasome pale (kwani ni wachache tu pale) yasiende makabila mengine. Kule mwanza samaki wauzwe mwanza kwa wasukuma tuu na pesa zipatikanzo zinufashe pale tuu. Mbuga za wanyama kaskazini pesa zitumike kaskazini tuu...n.k utaona mwisho wake utakuwa nini?
Maoni yangu lazima kuwe na makubaliano, usikilizano na mambo yawekwe hadharani. Kama gesi itaenda dar, nini kifanyike kwa wananchi wa mtwara na pembeni mwa bomba ili waone umuhimu wa kulinda makampuni na usalama?
Msitegemee maaskari bali mkae mjadili na mtende yatendeke.
kama huna la kuchangia ndugu yangu ni bora ukakaa kimya maana hujui kinajadiliwa nini,kwa faida yako na wasiojua wenzako ni hivi wanamtwara hawapingi kushea rasilimali na watanzania wengine la hasha,wanataka miundombinu yote ya gesi ijengwe mtwara kama kiwanda cha minofu mwanza au kiwanda cha kahawa kilimanjaro au viwanda vya makaa ya mawe mbeya nk.hapo ndipo gesi isafirihswe kama bidhaa na sio kama malighafi
Deletewa tz tuache siasa tufanye kazi ili tupate maendeleo kila jambo ni kupinga tu.uchochezi wa kisiasa unasababisha kurudisha maendeleo kwa ujumla nyuma.tufike mahali wa tz tuwatambue wanasiasa kua mtaji wao ni maneno ya uchochezi si vinginevyo wako tayali kwa lolote zuri au baya mradi tu wafanikiwe kisiasa
ReplyDeleteHAKUNA HATA MKAZI MMOJA WA MTWARA ANAEKATAA GESI ISIENDE DAR,KUNA VITU AMBAVYO VILIPANGWA KUJENGWA MTWARA VIMEFUTWA,MTAMBO MKUBWA WA MEGAWATI 300 KUINGIZA UMEME KATIKA GRIDI YA TAIFA LEO HAUPO TENA,VIWANDA VYA MBOLEA,SARUJI NK,VIJENGWE KWANZA HIVYO NDIVYO VYA KWANZA KUPANGWA NDIPO UINGIE VINGINE.
ReplyDeleteWanatafuta kuongeza idadi ya nchi duniani,
ReplyDeleteNi jambo la aibu kwa WAZIRI WA NCHI KAMA HUYU KUKURUPUKA KWA KIASI HIKI. Si vyema tukawa ni chanzo cha kumwagika kwa damu ya raia wetu kwa hoja zisizo na mashiko kwa kung'ang'aniza kitu ambacho hata mtoto anatambua uhalali wake. Kwani Dar es salaam au BAGAMOYO kuna nini hasa? Acheni kujidanganya nyie, hayo majeshi huwa yanafikia hatua yanashindwa pale raia wanapokuwa wamekata tamaa. ACHENI TAMAA ZA KIFISADI NYIE WAPENI WANANCHI WA KUSINI HAKI ZAO, MBONA WAMETESEKA KWA MUDA MREFU, AU MNAPENDA WAENDELEE KUITWA WAMACHINGA HUKO DAR?
ReplyDeleteSOMA MAONI YA WENZAKO KABLA YA KUCHANGIA SIO KUUZA SURA KWENYE GAZETI TOA MAONI YENYE TIJA
DeleteKUPELEKA GESI DAR SIYO KOSA,KOSA NI JE SERIKALI IMEELIMISHA WANANCHI WA MTWARA KWA NINI WAMEPELKA GESI DAR? KWANI KABLA YA KUAMUA KUFANYA MRADI WOWOTE KUNA MAMBO MENGI YANAZINGATIWA NDIPO MRADI UANZE,SIYO MAAMUZI YA MTU BINAFSI KUAMUA KITU FULANI KIFANYIKE WAPI,HIVYO NI JUKUMU LA SERIKALI KUWAELIMISHA WANANCHI SABABU HASA NI NINI,NA WAO WATAFAIDIKA VIPI,NA KAMA WANANCHI WANAJAMBO LA ZIADA WANATAKA SERIKALI WAWAFANYIE WAELEZE ILI SERIKALI IWEZE KULITOLEA UFAFANUZI.
ReplyDeleteKimsingi, wananchi wa Lindi,Mtwara na kusini yote kwa ujumla wanastahili kuhoji juu ya mpango wa usafirishaji gesi asilia kuelekea Dar es salaam, siyo tu kwa sababu mikoa hiyo imeonekana kutengwa kwa makusudi kutokana na mipango mibovu ya serikali lakini kwanza kwa sababu wanastahili kufahamu kama vile mtanzania yeyote anavyopaswa kufahamu juu ya mipango ya serikali yake.
ReplyDeletePili,kwa kuwa jukumu la serikali pia ni kuweka mazingira yatakayochochea maendeleo kwa watu wake siyo busara kwa viongozi kuondoa gesi huku kwa dhati wakijua kuwa wanaondoa kichocheo kikubwa cha maendeleo kwa ukanda wote wa mikoa ya kusini.
Tatu,hata ukiachilia mbali madai ya watu wa mikoa ya Lindi na Mtwara bado uamuzi wa serikali ya CCM haujazingatia kile ilichoandika katika katiba yake sehemu ya kwanza kifungu kidogo cha (4)kinachosema;Chama cha Mapinduzi kinaamini kuwa binadamu wote ni sawa,hivyo basi kisiondoe fursa za maendeleo zilizofungamana na gesi asilia, kufanya hivyo ni kukiuka inachosema inakiamini.
Hata katika kifungu cha (5)14 CCM inaamini kwamba matumizi ya utajiri wa Taifa yanatiilia mkazo maendeleo ya wananchi na hasa jitihada za kuondosha umaskini.....sasa serikali inafahamu hali duni ya maisha ya watu wa mikoa hii hivyo isingekuwa jambo la busara kuhamisha kichocheo hiki cha maendeleo kwao hasa kwa kuwa uwepo wake huko kusini hauzuii maeneo mengine ya Tanzania kunufaika na raslimali hiyo.
Hoja nyingine ni haja ya serikali kuheshimu mawazo, maoni na mapendekezo ya watanzania ambao ni wataalamu wa uchumi,gesi,madini,na hata walio wa kawaida kwa kuwa ndio walioiweka serikali madarakani,na kwamba ni wajibu wetu kama raia tunaoipenda nchi yetu kupendekeza namna mzuri ya kufanya maamuzi yatakayoimarisha umoja wetu.
Viongozi wa Serikali pia wazingatie misingi ya utawala bora (wanaifahamu na wanaihubiri wengine waizingatie),tumewapa dhamana,lakini haina maana kuwa wao ni wakamilifu kiasi kwamba hawawezi kupotoka kimtazamo,kimaamuzi(NOTE:EVEN WHEN ALL THE EXPERTS AGREE,THEY MAY WELL BE MISTAKEN).
Hivi ni raia wangapi wanaimani na selikari yao ya Kitanzania? wakati wengine wakitamka maneno makali kama "selikari gani yakibaguzi hii ya kuchukia Kusini" hadi baadhi ya mikoa wanajua kuwa Kusini kunakaliwa na watu wajinga.Leo hii selikari yetu inaona umuhimu wa elimu kwa jamii ya watu wa Kusini kuhusiana na suala zima la mradi wa GESI hali yakuwa iligundulika makarne yalopita. Hivi kumbe mtoto huwa anapenda pipi ilotiwa chumvi? ahadi za wanasiasa walomadarakani leo, zilikuwa ni kutupatia pipi ilotiwa sukari na juisi ya asali.Ila wanampango wa kutuletea sukari ya sumu. Nani asiyejua kua palipo na machimbo ya madini ya aina yoyote ile lazima kuwe na athari za mda mrefu?
ReplyDeleteWatu wanadhani kuwa yanayoongelewa na viongozi ni sahihi sana 'eti watu wa mtwara ni wachoyo na hawana elimu'.
WAMAKONDE hatujakataa kushea matumizi ya rasilmali gesi nchini kote (LA HASHA) ila,
Tunachotaka ni kwamba fursa za UWEKEZAJI lazima ziwekewe kipaumbele kwenye mkoa husika kwani athari tunazipata na ni zile za moja kwa moja sanjali na uchafuzi wa mazigira.
Hivi kwa nini uwekezaji ukafanyike KINYEREZI
hali ya kuwa MTWARA bado jamani? huoni kama ni uonevu?
Power plant station ikijengwa hapa Mtwara basi WAMAKONDE tutapata fursa za uwekezaji ikiwemo na kujengewa viwanda ili vijana wetu waokoke na adha ya ugumu wa ajira na kujikuta wanapata ajali za kupoteza viungo katika kazi za BODABODA.
Na kama hii haitoshi basi kama hamjui hapa Mjini kuna BONGE la DAMPO ambalo ni la sumu kali
'siku moja aliingia kenge ndani dampo hilo na kurudi akijikongoja mwisho alikufa'
Hizi athari tunazo sisi kwa nini uwekezaji ukafanyike Kinyerezi? kama tatizo ni GRIDI ya taifa ya umeme basi zipelekwe nguzo DAR na mikoa tumizi ya Umeme huo.
Lamsingi ni kuiombea nchi yetu ndugu maana. hii nchi imeshikiliwa na mikono ya watu wachache na hamna mtu mwingine anayesikilizwa. wakitaka kuipeleka gesi dar, watapeleka na apingaye atapigwa na kuuawa. hata hivo wako tayari kuua wananchi wote lakini wahakikishe kuwa maamuzi yao yametimia. TUIOMBEE SANA NCHI YETU MAANA TUENDAPO SASA NI VITA.
ReplyDelete