14 January 2013

RC aagiza ujenzi wa mabweni ya askari



Na Daud Magesa, Simiyu

MKUU wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Pascal Mabiti, ameuagizi uongozi wa Jeshi la Polisi mkoani humo, kujengwa kwa mabweni mawili ambayo wataishi askari polisi ambao hawajao.


Bw. Mabiti alitoa agizo hilo mwishoni mwa wiki katika hafla ya kuukaribisha mwaka mpya wa 2013, iliyoandaliwa na jeshi hilo mkoani humo kwa askari wake pamoja na wadau.

Akionesha kuguswa na tatizo la uhaba mkubwa wa nyumba
za kuishi askari pamoja na Maofisa wa jeshi hilo, Bw. Mabiti alisema ili kuondokaana na changamoto hiyo, askari wote na
wadau wa jeshi hilo wajitolee kwa hali na mali ili kufanikisha
ujenzi wa mabweni hayo haraka iwezekanavyo.

“Changamoto kubwa inayolikabili jeshi letu la polisi mkoani hapa ni upungufu wa makazi ya askari hasa wasio na familia na Maofisa wa ngazi za juu katika jeshi hili,” alisema.

Aliongeza kuwa, umefika wakati wa jeshi hilo kushilikiana na askari wake pamoja na wadau wao kuchangia ujenzi huo ili uweze kuanza haraka na wahusika kupata makazi ambayo yataongeza ufanisi wao.

Alimuomba Meya wa Mji wa Bariadi, atoe viwanja viwili vya kujenga mabweni hayo na kuahidi kutoa mashine ya kufyatua
matofali pindi ujenzi huo utakapokaribia kuanza

“Nawaomba wafanyabiashara wakubwa mkoani hapa, jitoleeni kuchangia ujenzi wa mabweni haya kwa kutoa mifuko ya saruji
ili kutenge makazi ya askari na Maofisa wa jeshi hili,” alisema.

Alimwagiza Kamanda wa Polisi mkoani humo, Salum Msangi, kufanya utaratibu ambao utafanikisha ujenzi huo ili kuwawezesha askari kupata makazi bora ili waweze kufanya kazi kwa uhur

No comments:

Post a Comment