21 January 2013

Pinda kufungua kikapu Zone V leoNa Amina Athumani

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda leo atazindua mashindano ya Kanda ya Tano ya mpira wa kikapu (Zone v)  katika Uwanja wa Ddani Taifa, Dar es Salaam.


Mashindano hayo yanashirikisha timu kutoka nchi 10 za Afrika huku Tanzania ikiwa mwenyeji wa michuano hiyo mikubwa kufanyika nchini.

Akizungumza Dar  es Salaam jana, Katibu Msaidizi wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Michael Maluwe alisema maandalizi kwa ajili ya mashindano hayo yamekamilika na mashindano hayo yatazinduliwa na Waziri Mkuu Pinda saa 9 alasiri.

Alisema kwa upande wa ufundi timu za Tanzania, Tanzanite King na Tanzanite Queens zimejiandaa vyema chini ya makocha wao wazawa, Bahati Mgunda na Evarist Mapunda wakisaidiwa na kocha wa kigeni kutoka nchini Marekani, Ocquis Sconiers ambaye ni kocha msaidizi pamoja na kocha mkuu Albert Sokaitis.

Mpaka jana timu zilizowasili kwa ajili ya michuano hiyo ni Somalia, Rwanda, Kenya, Uganda, Sudani, Sudani Kusini huku timu nyingine zikitarajiwa kutua leo asubuhi.

Alisema mechi za michuano hiyo zitaanza kuchezwa asubuhi isipokuwa mechi ya ufunguzi kati ya Tanzanite King na timu pinzani ambayo itachezwa kuanzia saa 9 alasiri.

No comments:

Post a Comment