28 January 2013

Nyamlani, Malinzi wawekewa pingamizi TFF



Na Zahoro Mlanzi

WAGOMBEA wote wa nafasi za juu za uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi Kuu Bara, wamewekewa pingamizi wasigombee uongozi kwa sababu mbalimbali.


Wagombea hao ni  Jamal Malinzi, Athumani Nyamlani wanaogombea Urais wa TFF, Michael Wambura anayegombea Umakamu Rais wa TFF, Yusuph Manji anayegombea uenyekiti wa bodi ya ligi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana na Ofisa Habari wa shirikisho hilo, Boniface Wambura iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah, ilieleza kwamba jumla ya pingamizi 14 zimewafikia tangu Jumatatu wiki hii hadi zoezi hilo linafungwa juzi.

 Alisema kwa upande wa uongozi wa TFF, Malinzi na Nyamlani wanaowania urais wamewekewa pingamizi, Wambura anawania umakamu rais pia naye amewekewa pingamizi pamoja na wagombea wa nafasi za ujumbe, Epatha Swai, Eliud Mvella na Athumani Kambi.

"Upande wa bodi, wagombea wa Uenyekiti Yussuf Manji, Ahmad Yahya Juma na Mgombea Umakamu, Mohamed Said nao pia wamewekewa pingamizi," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo ya Osiah.

Alisema Nyamlani amewekewa pingamizi mbili, moja na Mtanga Yussuf Gacha na nyingine ya Menard Justinian, wakati Malinzi amewekewa pingamizi moja na Agape Fuwe na Wambura ana pingamizi mbili, moja ya Osiah Samuel Msengi na nyingine ya Saidi Rubeya.

Aliendelea kueleza kwamba Epatha Swai amewekwa pingamizi na Ramadhan Sesso na Sos Chalamila, Eliud Mvella amepingwa na Saidi Kiponza, Abdul Changawa na Peter Namengi, wakati Athumani Kambi amepingwa na Jeremiah John Wambura.

Manji amewekewa pingamizi mbili, na mwanachama maarufu wa Simba, Daniel Tumaini Kamna na mwanachama wa Yanga, Juma Ally Magoma, Frank Mchaki amewawekea pingamizi Ahamd Yahya na Mohamed Said.

No comments:

Post a Comment