21 January 2013

Nitawachongea watendaji wote wa Halmashauri


Na David John.

MBUNGE wa Kisarawe Seleman Jafu amesema atahakikisha anawachongea kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda watendaji wote  wa halmashauri hiyo  ambao wanachangia kurudisha nyuma maendeleo ya wananchi wake.


Hayo aliyabanisha Dar es salaam jana wakati akizungumza na gazeti hili ambapa  alisema hatakuwa tayari kuona kisarawe inarudi nyuma kimaendeleo kwa ajili ya watendaji wazembe wachache ,wanaoshindwa kuwajibika vilivyo kwa wanakisarawe.

Jafu alisema kuwa kuna baadhi ya viongozi  wachache wa halmashauri hiyo wanashindwa kuwajibika katika nafasi zao hivyo anajipanga ili kupeleka taarifa hiyo kwa waziri mkuu  kuona namna gani wanaweza kushughulikiwa.


"Kama kiongozi anashindwa kwenda na kasi inayotakiwa  hasa katika kuona wananchi wa kisarawe wanapata matunda ya uwajibikaji wa wao,ambapo pia wameaminiwa na kuwapa majukumu ya kusimamia maendeleo ya mji huo alafu wanashindwa kufanya hivyo hakuna sababu ya kulifumbia macho tatizo hilo.'alisema

Aliongeza kuwa mapema mwezi huu alipokea malalamiko ya wananchi wa kijiji cha Visegese,kulalamikia halmashauri hiyo kushindwa kuezeka shule ya msingi kijijini hapo baada ya shule hiyo kuezuliwa na upepo makali (kimbunga)miaka mitatu iliyopita.

Akizungumazia hali hiyo Jafu alisema yeye kama mbunge kupitia mfuko wake wa Jimbo alishatoa fedha kwa ajili ya ukarabati wa shule hiyo ,lakini ameshangazwa kuona kuwa hadi leo shule hiyo bado haijakarabatiwa.

"Kuna haja ya kuwashughulikia viongozi ambao wanashindwa kuwajibika kwa wananchi kwani wanachangia kwa kiasi kikubwa kurudisha nyuma maendeleo ya wananchi na hasa wananchi wangu wa kisarawe."alisema

Mbunge huyo aliongeza kuwa niayake kubwa ni kutaka kuiona halmashauri hiyo inakuwa katika hadhi,na heshima ya hali ya juu na hasa kufuatia huko nyuma kusahaulika kimaendeleo,na kuonekana kama hakuna viongozi wanaowajibika kwa wananchi wao.

Aidha Jafu alihaidi kufuatilia suala la kusimamishwa kwa ujenzi wa kituo cha Afya kijijini hapo ambayo inajengwa kwa nguvu za wanachi ili kuona tatizo liko wapi. 

Awali gazeti hili lilimtafuta Mwenyekiti wa halmashauri ya Kisarwe na Diwani wa Kata  hiyo Adamu Nyimba ili kutaka kujua kuhusu malalamiko ya wananchi hao ambapo alisema hana kometi na kutaka atafutwe siku nyingine huku akiwaacha waandishi wa habari bila kupata ufumbuzi wa suala hilo.
No comments:

Post a Comment