03 January 2013

NBAA yatangaza matokeo

Jane Hamalosi na Christina Mokimirya

BODI ya Taifa ya Wahasibu na wakaguzi wa hesabu(NBAA)  imetangaza matokeo kwa watahiniwa wa mchepuo wa kwanza na wapili,cheti cha msingi,cheti cha kati na cheti cha hatua ya mwisho.


Taarifa hiyo ilitolewa jana na Mkurugenzi mtendaji wa Bodi hiyo Bw.Pius Maneno  alisema jumla ya watahiniwa 3853 waliofanya mitihani ya bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa hesabu (NBAA),Watahiniwa 703 ambao ni asilimia 18.2 wamefaulu na wengine 1332 ambao ni asilimia 34.6 watarudia somo au masomo waliyoshindwa na Watahiniwa 1818 ambao ni asilimia 47.2 hawakufaulu mitihani hiyo.

Pia ilisema katika ngazi ya mwisho Watahiniwa 173 ambao ni asilimia 15.6 kati ya 1,110 waliofanya mitihani hiyo wamefaulu na wengine 502 ambao ni asilimia 45.3 watarudia somo moja na watahiniwa 435 ambao ni asilimia 39.2 hawakufaulu.

Hata hivyo taarifa hiyo ilisema jumla ya Watahiniwa 188 wamefaulu shahada ya juu ya Uhasibu Nchini (CPA) idadi hii inafanya jumla ya Watahiniwa waliofaulu shahada ya juu ya uhasubu kufikia 4323 tangumitihani hii ianze mwaka 1975.

Aidha taarifa hiyo ilisema katika ngazi ya uandishi na utunzaji wa  hesabu Watahiniwa 23 sawasawa na asilimia 19.7 kati ya 117 wamefaulu na wengine 38 sawasawa na asilimia 32.5 watarudia somo moja au mawili na Watahiniwa 56 sawa na asilimia 47.9 hawakufaulu .

Hata hivyo idadi ya Watahiniwa waliofunzu ngazi ya uandishi na utunzaji wa hesabu  kufikia 3,372 tangu Bodi ilipoanza kutahini mitihani ya cheti hiki mwaka 1991.

No comments:

Post a Comment