21 January 2013

Nape afichua siri za kifo Chadema *Asema hakuna dawa ya kutumia lazima kife *Adai ni laana ya Nyerere, wasitafute mchawi


Na Mwandishi Wetu, Mwanza

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Itikadi na Uenezi, Bw. Nape Nnauye amekitaka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kisitafute mchawi anayewamaliza nje ya chama chao.


Alisema ubaguzi ulioota mizizi kwa muda mrefu ndio unaokimaliza chama hicho ambao umelelewa na waasisi pamoja na viongozi wa kitaifa hivyo kina haki ya kufa kutokana na dhambi hiyo.

Bw. Nnauye aliyasema hayo jana jijini Mwanza katika mkutano
wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Nyamagana.

Mkutano huo ulihudhuriwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Bw. Philip Mangula, baadhi ya Mawaziri na maelfu ya wananchi wa jiji hilo na vitongoji vyake.

Alisema matatizo yanayokikabili CHADEMA kutokana na dhambi inayofanywa na viongozi wake ambayo Hayati Mwalimu Julius Nyerere aliikemea na kudai ni sawa na kula nyama za mtu,
inakipa fursa chama hicho kuandaa mazishi kwani hakina jinsi
ya kujinusuru na kifo.

Alidai kushangazwa na viongozi wa CHADEMA kuendelea kukinyooshea kidole chama tawala na kudai kinahusika na
migogoro inayoendelea katika chama chao wakati CCM
iliwahadharisha mapema juu ya madhara ya ubaguzi.

“Sisi tuliwaeleza mapema kuwa, ubaguzi ambao wanaukumbatia licha ya kuathiri umoja na mshikamano ni dhambi inayoweza kukisambaratisha chama chao.

“Hamuwezi kuwa na chama ambacho kinaendekeza ubaguzi...ili kiongozi wake adumu na kuheshimika, lazima atoke ukanda fulani au ukoo fulani vinginevyo anasukiwa mizengwe na kutimuliwa.

“Walianza na marehemu Chacha Wangwe...hivi sasa wameanza kumuandama Zitto Kabwe (Naibu Katibu Mkuu CHADEMA),
na wanaoitwa vijana wake, nasikia wiki ijayo wamejipanga
kumfukuza John Shibuda (Mbunge wa Maswa Magharibi),
wiki ijayo,” alisema Bw. Nnauye.

Bw. Nnauye aliongeza kuwa, Mwalimu Nyerere aliwahi kusema dhambi ya ubaguzi ni kubwa hivyo chama hicho hakina jinsi ya kuachanana na ubaguzi unaoendelea.

Alidai kuwa, kama CHADEMA ambacho ni chama kidogo kinabaguana kiasi hicho, wakipewa dhamana ya kutawala
nchi hali itakuwa mbaya zaidi.

“Kama wanabaguana ndani ya kichama kidogo ambacho hakijai hata mkononi, watafanyaje wakipewa dhamana ya kuongoza hata kipande cha nchi yetu? Alihoji Bw. Nnauye na kudai kuwa, ubaguzi ndani ya CHADEMA umejikita kwenye ukanda, ukabila na udini

Alisema ubaguzi huo unajionyesha zaidi kwenye safu ya uongozi
wa chama chao na maeneo mengine ndio maana ameamua kuwapa ushauri wa bure ili wasiendelee kumtafuta mchawi nje ya chama.

20 comments:

 1. Ni bora umewaeleza ukweli. UBAGUZI ni HATARI SANA. Watanzania wenzangu, aidha uwe mwananchama wa chama cha siasa au la, kataa ubaguzi, kukataa kubaguliwa na wala usimbague mwenzako. Ninapatwa na hofu sana ninap[osubiri Uchaguzi Mkuu wa CHADEMA, Serikali za Mitaa 2014 na Uchaguzi Mkuu 2015. Tuiombee Tanzania na watu wake wote, walioko hapa nyumbani na kule nje. Mungu Ibariki Tanzania. Mungu

  ReplyDelete
  Replies
  1. hakuna jipya katika comment yako ubaguzi anaouzungumzia Nape upo ndani ya ccm muulize yeye Nape, Januari makamba ,Vita kawawa,shemeji Mwemwa,vick kamata,na wenzao waliojazana bot walifikaje hapo.Ama nawe unatumia makalio kuuona ukweli uliodhahiri.

   Delete
  2. Wewe gamba nani alikuambia CHADEMA kunaubaguzi kelele zote hizo ni kwasababu tunawanyima usingizi hamna uhakika wa kushinda 2015 wake zenu nccr na cuf pamoja na mtoto wenu adc mbona hamuwasemi kila kukicha CHADEMA ,CHADEMA mtasema sana sisi tunasonga mbele kusaka mabadiliko mkileta mapandikizi tunang'oa mara moja na sisi hatutakuwa wa kwanza kutoa mapandikizi NELSON MANDELA alimungo'a winnie alipogundua ni pandikizi la makaburu ambao hawakupenda mabadiliko kwasababu walinufaika na mfumo kama wewe unavyonufaika namfumo wa magamba.

   Delete
  3. CCM isipaniki tutawakomesha kwenye uchaguzi wa mitaa udiwani Ubunge na Uraisi CHADEMA ni chama cha wanyonge na wanyonge ndiyo wenye kupiga kura TUJIANDIKISHE

   Delete
  4. BR. John me nadhan hujaelewa ! ktk ukomboz wa tz hatuhitaj chama cha siasa kwani hata CHADEMA yenyewe hakika ina matatizo mengi tu, mbaya zaidi inatugwaw watz, xo cha msingi na cha secondari hakuna chama cha siasa kizuri hapo nashindwa kuelewa ubaguzi gn hamuuoni hapo,ndo ndo ile mnataka nafasi nanyi???? ACHENI IZO BN ACHENI KUWAPOTOSHA WATZ, By d way nia ya uvunjifu wa amani inaonekana waz nashaur tu jeshi la polisi kuwa makini hasa na vinara wa maandamano ya vurugu yenye kuondoa amani kwa maslahi ya wachache....UBAGUZI HAUKUBALIKI HATA KIDOGO

   Delete
 2. ni ukoo gani anaouzungumzia nappe zaidi ya ule unaoonyeshwa na, watoto wa vigogo ndani ya ccm kama vile;sioi sumar, hussen mwinyi, ridhiwani kikwete,makongoro.. na wengine wengi, ukweli siasa ni ya wote na chama razima kiwe na mwanzo na baadaye kusambaa nchi nzima,kwa miaka michache ya chadema na ile mingi ya ccm , ukoo unapatikana ccm, democrasia ya kweli hulindwa na katiba, anayevunja katiba apaswa kuadhibiwa kwa mjibu wa katiba.

  ReplyDelete
 3. IKO KAULI YA MZEE MAKAMBA KUWA PANYA WA MSIKITINI HULA MSAHAFU WAKATI YULE WA KANISANI HULA BIBILIA LA AJABU NI LIPI MBONA HUKO MAJUU GEORGE BUSH SENIOR NA JUNIOR WALISHIKA URAIS KWA VIPINDI TOFAUFI TANZANIA NI UMBEA NA UDAKU TU TUJIREKEBISHA

  ReplyDelete
 4. UPINZANI UTAKUWA KWA KUONYESHA MABAYA YA CCM, LAKINI KAMWE CCM HAITOKUWA KWA KUSHAMBULIA WAPINZANI, TAZAMA MTWARA, NAPE ALIKUJA NA STORI POLI KUHUSU CHADEMA, WATU WAKAKUMBUSHA AHADI NA KUTAKA MAJIBU YA MATATIZO YAO, CCM HAWAKUWA NA MAJIBU WAKAISHIA KUZOMEWA TU, CCM IJIPANGE KUZIMA MOTO KWA KUWA MOSHI UPO TAYARI

  ReplyDelete
 5. Haya niambie nani anatoa vyeo kwa ukoo naanza na ccm ni VITA KAWAWA(MB) ZAINABU KAWAWA(MB) SALMA KIKWETE(MJUMBE MKUTANO MKUU ALIPITA BILA KUPINGWA) RIDHIWANI KIKWETE (MJUMBE MKUTANO MKUU ALIPITA BILA KUPINGWA) NAPE NAUWE(K/MWENEZI) KHALFANI KIKWETE(KAMANDA WA CHIPUKIZI TANZANIA) DR HUSSEIN MWINYI(WAZIRI) SAIDI MWEMA IGP(HUYU NI SHEMEJI) HAWA GHASIA(WAZIRI)HUYU NI SHEMEJI JANURI MAKAMBA (WAZIRI) WADAU WENGINE SIWAKUMBUKI NAOMBA MNIKUMBUSHE,PIA NAOMBA ORODHA YA CHADEMA FAMILY

  ReplyDelete
 6. NAPE NA CCM KUWENI MAKINI MISIKITI NA MAKANISA INACHOMWA MOTO SABABU YA KAULI ZENU WANA CCM ANGALIA 2010 KIKWETE ALIMPINGA SLAA KISA ALIKUWA PADRE NA KUTAKA ASICHAGULIWE.UZURI MMOJA DOKTA ALISEMA HAENDI IKULU KUWA ASKOFU AU SHEHE.ONA MIGOGORO YA DINI ILIYOPO NI KUTOKANA NA KAULI ZENU CCM MF,MSEKWA IGUNGA,MWIGULU ARUMERU NA KIKWETE NCHI NZIMA 2010 KUWENI MAKINI CCM WATANZANIA TUNAONA.SASA MMEKUJA NA SERA KWAMBA CHADEMA NI CHAMA CHA UKANDA(UCHAGA)ACHENI PROPAGANDA TUNATAKA MELI ALIYOAHIDI KIKWETE 2010 ZIWA VICTORIA,NYASA,NA AHADI NYINGINE.PESA ZA EPA TUJUE WALIOZIRUDISHA KWA RAIS USIKU NA ZIPO WAPI.NA UWAJIBIKAJI.AU KAMA UPINZANI HAUTAKIWI WAFUTENI.AU VISEMENI PIA VYAMA VYA CUF,NCCR N.K.WATANZANIA KUMBUKENI MFA MAJI HAACHI KUTAPATAPA MA MTI WENYE MATUNDA SIKU ZOTE NDIO UNAOPIGWA MAWE.ILA UDINI ULIOPO NCHINI NA KUBAGUANA CHANZO NI CCM KATIKA KUWAKABILI CHADEMA.JIULIZE MBONA SIJASIKIA SLAA,MBOWE,ZITTO,ARFI N.K. WAKIONGELEA UDINI,UKABILA.UKANDA ISIPOKUWA UTAMSIKIA KIKWETE,MWIGULU,NA MPIGA DEBE ASIYEPATA WASAFIRI NNAUYE.(aliyeuza utu wake kwa kupewa ukuu wa wilaya)SERA YA KUJIVUA GAMBA IMEISHIA WAPI KIJANA MWENZANGU MBONA MAGAMBA BADO YANATESA MKISHINDWA KUWAONDOA WANANCHI TUTAWAONDOA 2015 WEWE NA MAGAMBA WENZAKO WABUNGE,MADIWANI WA CHADEMA ENDELEENI KUTUSIMAMIA SISI WANANCHI MASKINI MAANA CCM LAO MOJA MUNGU IBARIKI CHADEMA MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WANANCHI WAKE.

  ReplyDelete
  Replies
  1. hakuna mungu wa kubariki vyama vya siasa mpendwa , kama vyama vya siasa vinasababisha uhai wa wa2 kutoweka ni mungu gn wa kubariki upuuzi huo! TUMWOMBE MUNGU TU TUPATE WATU TOFAUTI WALA C WANASIAS KAMA UNAVOFIKIRIA KIRAHISIRAHISI IVO....MWENYE BUSARA HAWEZI KUUNGA MKONO YANAYOFANWA KISIASA NCHINI,

   Delete
 7. tatizo la Nape ni kufikiri kinyumenyume na kweli masaburi hakukosea kuwa ndani ya ccm kuna viongozi wanafikiri kwa kutumia makalio

  ReplyDelete
  Replies
  1. WALIOTUKANA NA WABUNGE WOTE WA DAR-ES SALAAM WAKIWEMO WA UPINZANI MPAKA LEO WAMESHINDWA KUMUSHITAKI KWANI NI KWELI

   Delete
 8. nape mhafidhina wewe anayoyasema ni KELELE ZA MFWA MAJI hazitunyimi usingizi hata kidogo na wala haziwabadilishi WATANZANIA kuiacha CHADEMA tunasonga mbele kusaka mabadiliko.

  ReplyDelete
  Replies
  1. HIVI JAMII FORUM LICHA YA PEW RESEARCH CENTRE YA MARIKANI KUWATUKANA KUWA ASILIMIA 93 YA WATANZANIA NI WASHIRIKINA,WAVIVU WA KUFIKIRI, WAMESHINDWA KUSUGUA BONGO HATA KWA MAMBO MADOGO WENZENU WAKIONGOZA KWA ICT AFRIKA HAPO JIRANI HIVI KWENYE SOKO LA AJIRA LA AFRIKA MASHARIKI NI NANI ATAAJIRI VUVUZELA WASHIRIKINA JE MUNAFAHAMU HIZI NI ENZI ZA UTANDAWAZI ,UTANDAZUZU NA UTANDAWIZI ?????????

   Delete
 9. Huyu nape hakuropoka jamani, na tusimjibu kwa hasira, aliyoyasema yapo, hivyo kama ni kweli wanachadema tunataka kujisafisha na kuleta demokrasi ya uhakika haya aliyoyasema napoe tuyafanyie kazi badala ya kukebehi

  ReplyDelete
 10. CHADEMA bado itaendele kupwendwa CCM endeleeni kukumbatia ufisadi cha moto mtakiona hatutaki kofia zenu na vitenge vyenu

  ReplyDelete
 11. NAPE tueleze utekelezaji wa ahadi zenu, mambo ya CHADEMA waachie wenyewe. mbona ninyi mmeshindwa kuvuana magamba ? acha unafiki.

  ReplyDelete
 12. nape unakosea sana unnaposhindwa kutueleza ukweli wa chama chako kama katibu mwenezi wa chama na kuzungumza mambo mengi ya chama kingine. JE CCM NA CHADEMA kipi kinaangamia? don lie us we know all that are PROPAGANDA.Unatudananyaaaa:ni azan

  ReplyDelete
 13. ACHA UNAFIKI KIJANA NAPE NNAUYE!! KABLA YA UCHAGUZI MWAKA 2010,WEWE,SITA NA MWAKYEMBE MLIKUWA NA MPANGO WA KUHAMA CCM NA KWENDA CCJ AU CHADEMA!!!

  ReplyDelete