03 January 2013
Mwalimu ajinyongwa kwa msongo wa mawazo
Na Theonestina Juma, Kagera
MWALIMU wa Shule ya Msingi Mushisho, iliyopo katika Wilaya ya Kyerwa, mkoani Kagera, Medadi Rwabiga, amefariki dunia baada ya kujinyonga na kuacha ujumbe unaosema, amechukua uamuzi huo kutokana na msongo wa mawazo yanayomkabili.
Habari zilizolifikia gazeti hili, zinasema tukio hilo limetokea Desemba 30,2012, saa nne asubuhi, ambapo Rwabiga alijinyonga kwa kamba aliyoifunga katika mti uliokuwa jirani na nyumba yake.
Kamanda wa Polisi mkoani humo, Phillip Kalangi, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa, Desemba 2011, Rwabiga alifanya jaribio la kujiua kwa kunywa dawa ya kuoshea mifugo.
“Katika jaribio hilo, hakufanikiwa kujiua baada ya kuwahishwa hospitali na kupewa matibabu yaliyoondoa sumu aliyoinywa lakini inaonesha bado alikuwa na dhamira ya kujiua,” alisema.
Kamanda Kalangi alisema hadi sasa hawajajua chanzo cha mwalimu huyo kuchukua uamuzi huo hivyo wanaendelea na uchunguzi zaidi na ameacha mke, watoto wanne.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment