21 January 2013

Mmoja afariki dunia, watano wajeruhiwa Dar


Na Leah Daudi

MTU mmoja aliyefahamika kwa jina la Hatibu Halfani (33) amefariki dunia mara baada ya gari alilikuwa akiendesha  kugongana na gari lingine na kumsababishia kifo.


Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa Mkoa wa kipolisi Kinondoni Charles Kenyela alisema tukio hilo lilitokea juzi katika maeneo ya mbezi Afrikana Kinondoni.

Kamanda Kenyela alisema gari namba T 377 AKB Nissan ikiendeshwa na Saimoni Cosmas(35) ikitokea Tegeta kuelekea Kawe aligongana uso kwa uso na gari namba T 707 BYV aina ya Suzuki iliyokuwa ikiendeshwa na Hatibu Halfani (33) mkazi wa Tegeta akitokea Kawe kuelekea Tegeta.

Alisema katika ajali hiyo dereva wagari namba T 707 BYV alifariki dunia papo hapo na majeruhi 6 wa gari namba T 377 AGB waliumia sehemu mbalimbali za miili yao.

Kamanda Kenyela alisema dereva wa Nissan Civilian amelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili na majeruhi wengine watano.

Wakati huo huo huko maeneoa ya Mabibo Kinondani askari walifanya msako na kufanikiwa kuwakata watuhumiwa 15 wakiwa na pombe haramu aina ya gongo lita 100.

Kamanda wa Mkoa wa kipolisi Kinondoni aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Aziza Athumani (42) Rashidi Salimu (28) Masumbuko Masesa(35) Fatma Juma (20) Rahimu Shabani (28) na wenzao 10. 

No comments:

Post a Comment