14 January 2013
Mkandarasi soko la Mwanjelwa adaiwa kushindwa kazi
Na Esther Macha, Mbeya
UJENZI wa Mradi wa soko la wafanyabiashara wadogo unaoendelea eneo la Mwanjelwa Jijini Mbeya ,unadaiwa kukwama,baada ya mkandarasi aliyepewa zabuni ya ujenzi wa soko hilo –TANZANIA BUILDINGS WORKS-TBW kwa gharama ya zaidi ya Bilioni 12 anadaiwa kushindwa kazi.
Kazi ya ujenzi huo wa soko imeanza kujengwa mwaka 2010 miaka miwili baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete kukabidhi hundi kwa halmashauri ya Jiji la Mbeya Oktoba mwaka 2008 kama mkopo kutoka Benki ya CRDB.
Hata hivyo Mkandarasi huyo TANZANIA BUILDINGS WORKS alipewa zabuni na Halmashauri ya Jiji la Mbeya,ambaye ameanza ujenzi wa soko hilo Agost 25 mwaka 2010,kwa mujibu wa mkataba wa ujenzi wa soko hilo miezi 18 .
Akizungumza jana mara baada ya Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa serikali za mitaa Hawa Ghasia ,Meneja mradi wa kampuni ya ushauri ya mradi wa ujenzi wa soko la Mwanjelwa Bw.Liberate Materu alisema pamoja na kuwa mkandarasi huyo kulipwa fedha za walipa kodi zaidi ya Bilioni 8 lakini soko hilo halijakamilika mpaka sasa .
Hata hivyo kitendo cha kutokamilika kwa ujenzi huo kimemtia hofu Waziri Ghasia na kusikitishwa na kusua sua kwa ujenzi wa soko hilo,linalosubiriwa na wananchi.
Aidha Soko hilo lilitakiwa likamilike ujenzi.agost 24 mwaka 2011 na mkandarasi huyo kukakabidhi jengo kwa mwajili wake Halmashauri ya Jiji la Mbeya,.
Hata hivyo ujenzi huo umekamilika kwa asimilia asilimia 68 ya gharama zote,inadaiwa amefikia asilimia 70 na ameshindwa kumalizia asilimia 30 ya ujenzi iliyobakia.
Hata hivyo Mkuu wa MKoa wa Mbeya Bw. Abbas Kandoro alisema serikali imetoa fedha lakini baadhi ya watu wachache wameendelea kuiangusha.
Mkurugenzi wa Halmashaurii ya Jiji la Mbeya Bw. Juma Idd amekiri kuwa pamoja na kushindwa kazi kwa mkandarasi huyu ,lakini pia hayupo eneo la ujenzi wa soko kwa muda mrefu sasa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment