14 January 2013

Finland watoa Dola milioni tano nchini



Na Rehema Maigala

SERIKALI ya Finland kupitia ubalozi wake nchini imetoa dola milioni tano kwa ajili ya tume inayorekebisha sera ya tehama hapa nchini.


Tume hiyo ambayo imetoka Wizara ya Sayansi na Tekinolojia ambayo kwa hivi sasa wapo katika mchakato wa kurekebisha sera hiyo kuwa ya kisasa zaidi.

Akizungumza na waandishi wa Habari Mkurugenzi wa DBTi George Mulamula alisema fedha hizo zitawasaidia watu wanaorekebisha sera ya TEHAMA hapa nchini.

Hayo alisema katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia katika kitengo chake cha Mkakati wa Ubunifu wa Biashara (DBTi).

Alisema kuwa Serikali ya Finland itatoa pesa hiyo kwa ajili ya mipango ya miaka mitatu ijayo.

Katika warsha hiyo Mulamula alisema kuwa Serikali hiyo ipo tayari kusaidia na kuendeleza katika fani ya Tekhama na ujasiriamali.

Hata hivyo alisema ushirikiano wao na Serikali hiyo itasaidia zaidi kujifunza mbinu mbalimbali za ujasiriamali.

"Wajasiliamari wengi wakishindwa wanaacha kinachotakiwa si kuacha bali ni kukaa na kubuni mradi gani wa kufanya"alisema Mulamula.

Hata hivyo alisema kuwa kwa sasa wamewekeza mfuko wa kujikimu ambao una pesa dola laki moja kwa ajili ya wajasiliamali ili waweze kuendeleza bioashara zao.

Naye, Balozi wa Finland nchini Tanzania Sinikka Antila alisema kuwa,ujasiriamali unaleta maendeleo na ndio chanzo kikubwa cha kuleta ajira .

"Ujasiriamali unasaidia kuondoa umasikini na unafanya kuwa na maisha ya uwakika kila wakati"alisema Antila.

Vile vile alisema Serikali yao imekuwa ikisaidia sekta binafsi chini ya ushirikiano wake wa maendeleo na imekuwa ikijumuisha juhudi za kusaidia mazingira mazuri ya ubunifu. 


No comments:

Post a Comment