21 January 2013

Marufuku korosho kununuliwa kwa vipimo vya kangomba-DC



Na Steven Augustino, Tunduru

MKUU wa Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma, Bw. Chande Nalicho amepiga marufuku ununuzi wa kutumia Vipimo vya KANGOMBA chenye ujazo wa zaidi ya kilo moja unaoendelea sasa kutokana na kuwanyonya wakulima wa Korosho.


Wito huo umetolewa kufuatia kikao cha Baraza la Ulinzi la Usalama la Wilaya hiyo lililoketi kwa ajili ya kuthimini hati ya zao hilo kwa wakulima hao.

Akifafanua taarifa hiyo Bw. Nalicho alisema kuwa sambamba na maelekezo hayo pia Serikali kwa kushirikiana na Uiongozi wa Chama Kikuu cha
Wakulima wa Wilaya hiyo, (TAMCU) kimeunda Tume ya watu 7 ambao wataenda kuonana na waziri wa Kilimo na Chakula kupata kauli ya mwisho juu ya hati ya Korosho hizo ambazo hadi sasa bado hazijaanza kununuliwa.

Bw. Nalicho aliendelea kueleza kuwa Tume hiyo inatarajia kwenda kuomba huruma ya Serikali ili iwadhamini kutokana na Chama hicho kukosa sifa
za kukopesheka baada ya kushindwa kurejesha deni la Benki la zaidi ya shilingi Bilioni.2.8 kati ya fedha zilizokopa msimu uliopita.

Alisema ili kudhibiti hali hiyo viongozi wa Serikali za Vijiji,viongozi wa Vyama vya ushirika na halmashauri wanatakiwa kuunganisha nguvu zao ili kulinda mipaka yake katika njia zinazotoka na kuingia wilayani humo na kuhakikisha kuwa hata punje moja ya Korosho haitoroshwi.

Wakati hayo yakiendelea upande wa Viongozi wa Vyama vya Ushirika vya msingi vya wakulima wanasema kuwa amri hiyo ni danganya toto kwa madai kwamba ni kweli halmashauri hiyo inawatoza Ushuru wa Shilingi
60 kwa kilo za korosho hizo zinazo nunuliwa kinyemela.

Alimtupia lawama za moja kwa moja Mkurugenzi Mtendajiwa halmashauri ya Wilaya hiyo kuwa ndiye kikwazo na hajawajibika ipasavyo.

Akijibu tuhuma hizo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bw. Robert Nehatta alisema kuwa tuhuma hizo siyo za kweli kwa madai kuwa yeye
alikwisha toa maelekezo ya kuzuwia ununuzi huo kupitia barua kumbu kumbu namba TDC.C.20/vol.11/14 ya Desemba 22 mwaka jana.

Alisema katika barua hiyo ambayo ilipelekwa kwa maafisa watendaji wa vijiji wote Wilayani humo na nakala zake alizipeleka kwa Mkuu wa Wilaya, Mkuu wa polisi, mwenyekiti wa halmashauri na madiwani wote
pamoja na mambo mengine aliwaomba kutoa msaada na usimamizi mkubwa wa udhibiti wa wanunuzi hao.



No comments:

Post a Comment