07 January 2013
Manispaa Songea yapanda miti 70,000
Na Joseph Mwambije, Songea
MANISPAA ya Songea Mkoani Ruvuma imepanda jumla ya miti 70,000 tangu mwaka 2000 ilipoanza kampeni ya upandaji wa miti na Januari 2,mwaka huu imepanda miti 3500 katika siku iliyoteuliwa kuwa ya upandaji miti katika halmashauri hiyo.
Hayo yamebainishwa jana na ofisa wa misitu wa manispaa hiyo Bw.Robert Mgowole wakati akizungumza kwenye kampeni ya upandaji miti kwenye chanzo cha maji cha Ruhila na kubainisha kuwa manispaa hiyo ina vyanzo vya.
Alisema kuwa kuna vyanzo 38 vya maji katika manispaa hiyo na kwamba vilivyopandwa miti ya kuhifadhi maji ni 20 kati ya vyanzo hivyo 38 na kwamba miti mingine 10,000 itaendelea kupandwa kweny vyanzo vingine.
Kwa upande wake Meya wa Manispaa ya Songea Mkoani humo Bw.Charles Mhagama alitka kasi ya upandaji miti iendane na kasi ya utunzaji na kuongeza kuwa kila mtu ni mdau wa mazingira hivyo akawataka wananchi kutunza miti na vyanzo vya maji.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na usafi wa Mazingira Songea (SOUWASA) Mhandisi Wilson Mandia alisema kuwa mwaka jana kulikuwa na tatizo kubwa la maji kutokana na uharibifu wa mazingira na kuwataka wananchi kutunza vyanzo vya maji.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment