07 January 2013

Waumini parokia ya Muheza wapewa somo


Na Steven William,Muheza

PADRI wa Kanisa Katoliki Parokia ya Muheza mjini wilayani Muheza Martini Kihiyo amewataka waumini wa kanisa hilo kumchukuru Mungu kwa kuweza kuwafikisha kuuona mwaka mpya.


Hayo yalisemwa na padri huyo katika ibada ya mkesha wa sikukuu ya mwaka mpya katika kanisa hilo ambapo alisema kuwa ni lazima waumini wajiulize watamtolea sadaka gani Mungu kwa kuwa amewavusha salama kwa kipindi mwaka uliopita.

"Inatakiwa waumini tujiulize kwamba mwaka uliopita nilifanya nini ama nilipata matatizo gani ama maendeleo na kumtolea sadaka,"alisema.

Padri Kihiyo alisema kuwa kuna watu wengine wameingia katika mwaka mpya wakiwa na matatizo kama vile kufungwa jela,kuumwa,kufa,kunywa pombe n kuoita kiasi na matatizo mengine mengi.

Alisema kuwa endapo hadi sasa kama kuna mtu ambaye hakupata tatizo lolote ni jambo la kumshuruku Mungu kwani wengi wanamaliza mwaka bila ya kupatwa na matatizo.

Aidha padri huyo aliwataka waumini hao kuwaombea waumini wengine ambao hawana nafasi hata ya kumuomba Mungu na hata ukiwaeleza juu ya utoaji wa asilimia kumi kwenye mishahara yao huwa ni ugomvi.

"Kuna watu wamejitokeza kuwaua watu wengine kwa sababu wanaamini watapata thawabu jambo ambalo si la kweli bali ni kutawaliwa na shetani, hivyo pia tutumie nafasi hii kuwaombe wasiokuwa na nafasi ya kufika na kutoa sadaka, " alisema.

Alisema kuwa watu wanachoma makanisa wakizania watapata thawabu kwani hao hawajui watendalo na Mungu atawasamehe na kuongeza kuwa hali ya mifarakano isipenye katika nchi yetu.


No comments:

Post a Comment