14 January 2013

Kinyela ashutumu operesheni kamata changudoa Temeke


Na Kassim Mahege.

SIKU chache baada ya Kamanda wa Mkoa wa kipolisi Kinondoni Bw.Charles Kenyela kufanya Operesheni ya Kuwakamata wanawake wanaojiuza,Kamanda wa Temeke Bw.Engelbert Kiondo ameishutumu vikali Operesheni hiyo.


Akizungumza na gazeti hili jana alisema kuwa Kamanda Kenyela amefanya Operesheni hiyo kwasababu hakutaka kuisoma Elimu ya jamii ya madanguro na kuielewa na kuongeza kama angeisoma asingekurupuka kufanya Operesheni hiyo.

"Ukisoma Socialogy ya madanguro,haitaji Operesheni yoyote ile.Kamanda Kenyela hakupaswa kuwakamata na kuwabughudhi watu wale,wakati sheria ya kumshitaki hakuna,"alisema.

"Kuna mantiki gani ya kuwakamata watu hali ya kuwa hakuna kipengele kinachompelekea kumshitaki?halafu ukimkamata ndio inakuwa nini?"alihoji.

Kamanda Kiondo akifafanua kuhusu sakata hilo alisema hakuna sheria ya kumshitaki mtu anayeuza mwili wake isipokuwa kuna sheria ya kumshitaki mtu anayetoa jengo lake ili litumike kama danguro na kuongeza kuwa sio kumkamata mtu anayeuza mwili wake.

"Sasa unamkamata mtu anayeuza mwili wake tokea ulipoanza kusoma hebu niambie wapi umesikia sheria hiyo,"alihoji.

Alisema uwepo wa Madanguro unatokana na uhitaji wa jambo hivyo kuna watu wanahitaji jambo hilo na kusisitiza kuwa kama kusingekuwepo na uhitaji wa jambo hilo kusingekuwepo madanguro.

Alisema njia mbadala ni kuwapatia elimu ya kutosha watu wote wanaojiuza miili yao,kutokana na maradhi yanayopatikana kwa ajili ya kazi hiyo ikiwa ni pamoja na kuwashauri kubuni njia nyingine mbadala ya kujitafutia riziki zao za halali.No comments:

Post a Comment