03 January 2013
JK amteua Lyimo M-kiti mpya TASAF
Na Grace Ndossa
RAIS Jakaya Kikwete, amemteua Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Peniel Lyimo, kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), kwa kipindi cha miaka mitatu.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefua, ilisema uteuzi huo ulianza Desemba 20,2012.
Alisema wajumbe waliochaguliwa katika kamati hiyo ni Dkt. Khalid Salum Mohamed (Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar), Bw. Amran Masoud Amran (Ofisa Mdhamini Pemba, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Zanzibar), Bw. January Kayumbe kutoka Idara ya Umwagiliaji, Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika.
Wengine ni Bi. Winfrida Nshangeki (Mkurugenzi Idara ya Serikali za Mitaa, TAMISEMI), Bi. Nyancheghe Nanai (Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu), Bw. Ally Ahmed (Mkurugenzi Msaidizi Soko la Ajira, Wizara ya Kazi na Ajira), Bi. Constansia Gabuse (Mkurugenzi Msaidizi, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto).
Aliwataja wengine kuwa ni Bi. Ened Munthali (Mratibu wa Sera na Mipango, Ofisi ya Rais, Ikulu), Bi. Mariam Mchumi (Mkuu, Idara ya Sera na Mipango, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii), Bw. Hussein Mativila (Mhandisi, Wizara ya Ujenzi) na Bw. Jerome Buretta, (Kamishna Msaidizi, Fedha za Nje, Wizara ya Fedha).
Wengine ni Bw. Zuberi Samataba (Mkurugenzi, Elimu ya Msingi, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi) na Bw. Abbass Kandoro ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment