14 January 2013
Dkt. Shein asamehe wafungwa 16 Z'bar
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein, jana ametoa msamaha kwa wafungwa 16 ambao ni wanafunzi wa Chuo cha Mafunzo, kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 49 ya Mapinduzi, yaliyofanyika Januari 12,1964.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Ikulu Zanzibar, ilisema Dkt. Shein ametoa msamaha huo kwa mujibu wa uwezo aliopewa kisheria chini ya kifungu namba 59 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
Msamaha huo hutolewa kila mwaka katika kipindi cha sherehe za Mapinduzi kwa kuhusisha wafungwa ambao ni wazee sana, wenye maradhi sugu, wenye vifungo vidogo vidogo na walioonesha nidhamu nzuri chuoni.
Wafungwa wenye makosa kama ya wizi wa kutumia nguvu, kuiba maliza Serikali, kudhalilisha wanawake, watoto na dawa za kulevya huwa hawapewi msamaha.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment