07 January 2013

Chanjo ya kichomi,kuharisha ni salama-DC


Na Damiano Mkumbo,Singida

MKUU wa Wilaya ya Singida Queen Mlozi amewahakikishia wazazi na walezi wa watoto wadogo kuwa chanjo mpya dhidi ya ugonjwa kichomi na kuharisha zinatolewa kwa watoto wadogo ni salama .

Mlozi alisema alitoa Rai hiyo wakati wa uzinduzi wa chanjo mpya mbili za kuwakinga watoto waliyo nchini ya miaka mitano dhidi ya magonjwa hayo uliyofanyika kituo cha Afya cha Sokoine Halmashauri ya Singida juzi.

Mkuu huyo wa Wilaya chanjo hizo zitatolewa zote pamoja na zile za awali bila kuharibu ubora wake  na ni salama hazina madhara yoyote kwa binadamu.

“Chanjo ya aina ya Rotarix inayokinga ugonjwa wa kuharisha itatolewa mara mtoto anapofikisha umri wa wiki sita baada ya kuzaliwa naya pili baada ya wiki ya 10 atakapo kamilisha zote “ alisema Queen Mlozi.

Aliendeleza kueleza kuwa chanjo aina ya PVC 13 inakinga ugonjwa wa Kichomi pia inatolewa kwa watoto anapofikisha umri wa wiki sita baada ya kuzaliwa ikiwa ni dozi ya wiki ya sita ya pili wiki 10 na kukamilisha dozi ya tatu wiki ya 14.

Alihimiza kila mzazi au mlezi kumpeleka mtoto wake kupata chanjo inayostahili kwenye kituo chochote kinachotoa huduma za chanjo ambacho kipo karibu naye.

Katika kufanikisha zoezi hilo aliwataka viongozi na watendaji wa Serikali, vyama vya siasa, madhehebu ya dini, taasisi na wadau wote wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida kuhakikisha kuwa jamii inapata taarifa sahihi juu ya ratiba ya chanjo hiyo.

Akitoa maelezo juu ya zoezi hilo mganga mkuu wa Halmashauri ya Manispaa hiyo Dkt. Abdalla Dihenga alisema Serikali imeazimia kwa makusudi kutoa chanjo hizo mbili kutokana na matatizo waliyopata watoto.

Aliongeza kuwa utafiti uliofanyika uligundua kuwa vifo vingi vya watoto chini ya miaka mitano vinatokana na upungufu wa maji mwilini hali iliyosababishwa na ugonjwa wa kuharisha na  kichomi.

Katika uzinduzi huo uliyohudhuriwa na vuongozi mbalimbali wataalam wa Afya na wazazi wa akiwepo stahi Meya wa Manispaa ya Singida Salumu Mahami watoto watu walichanjwa ambao ni Basil Gaspar, Godfrey Stephano na Amina Ramdhani.

Kauli mbiu ya zoezi  hilo ni “mtoto asiyechanjwa ni hatari kwake mwenyewe na wengine, mpeleke apate chanjo”.

No comments:

Post a Comment