07 January 2013

Agakhan yazindua mradi kuboresha huduma afya


Na Jesca Kileo

HOSPITALI ya Agakhan imezindua mradi mpya ya kuunganisha mikono kwa ajili ya kuboresha huduma afya ya mama mjamzito na watoto Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi jijini Dar es Salaam Mkuu wa Uratibu hospitalini hapo, Amini Habibu alisema mradi huo unatekelezwa na Agakhan Foundation kupitia kituo cha huduma ya afya Agakhan.

Alisema kuwa katika uboreshaji huo umeanzia katika mikoa mitano ambayo inaongoza kwa vifo vya akina mama wajawazito na watoto ambayo ni Mwanza, Dodoma, Iringa, Mbeya na Morogoro.

Alisema washiriki wengine katika utekelezaji wa mradi huo ni ni MoHSW,AKHST,AKU na wadau wengine kwenye jamii katika kuhakikisha hakuna mama mjamzito atakayekuwa anafariki wakati wa kujifungua na wala mtoto atakayefariki kwa magonjwa yanayozuilika.
                       
Bw.Habib alisema lengo lao kubwa ni kuhakikisha wanaboresha kiwango cha upatikanaji wa huduma ya afya ya mama mjamzito na watoto,kuongeza kiwango  cha matumizi ya huduma ya afya ya mama mjamzito na watoto.

"Ili huduma hii iweze kufikia malengo tumeona tuweke magari ya wagonjwa ambayo yatasaidia kuwabeba wagonjwa ambao watakuwa hawajiwezi ili kuwawezesha kuwahi katika vituo vya afya,"alisema.

Mkuu wa mradi huu Sisawo Konteh alisema kupitia huduma ya magari hayo watakuwa watahakikisha kuwa inafanya kazi kwa kuzingatia muda katika ngazi ya wilaya na vituo vya afya vingine.

Aidha Konteh alisema huduma hiyo itaendelea kutolewa bure kwa ushirikiano wa mpango wa Serikali wa kufikia malengo ya millenia.

No comments:

Post a Comment