03 December 2012
Zito kuwasha moto Geita leo
Na Faida Muyomba, Geita
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Zitto Kabwe, leo atahutubia wakazi wa mji
wa Geita na kuwapokea wanachama wapya 50 kutoka Chama
Cha Mapinduzi (CCM), ambao watajiunga na chama hicho.
Akizungumza na gazeti hili, Katibu Mkuu wa CHADEMA, wilayani humo, Bw. Rogers Luhega, alisema Bw. Kabwe ataongozana na mbunge wa Nyamagana, Bw. Ezekiel Wenje.
Alisema miongoni mwa wanachama wapya ambao watajiunga na chama hicho ni pamoja na Mwenyekiti wa zamani wa CCM wilayani humo ambapo mkutano huo utafanyika katika
Viwanja vya Magereza.
“Mkutano huu utaanza saa tisa alasiri kwa lengo la kuimarisha chama ambapo Bw. Kabwe atapokea anachama zaidi ya 50, akiwemo Bw. Ntinonu (Mwenyekiti wa zamani wa CCM
wilayani Geita),” alisema Bw. Luhega.
Akizungumza na Majira, Bw. Ntinonu, alisema yeye na waliokuwa wanachama wenzake wa CCM, wakiwemo viongozi wanne wa matawi na kata, wameamua kwa hiari yao kuhamia CHADEMA baada ya kuchoshwa na vitendo vya ufisadi katika chama tawala.
'”Kesho (leo), tunahamia rasmi CHADEMA na kukabidhiwa kadi mpya kwani tumechoshwa na ufisadi uliokithiri ndani ya CCM ambao umesababisha kupatikana kwa viongozi wabovu,” alisema Bw. Ntinonu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment