17 December 2012
Yono: Nagombanishwa na Mangula
Na Eckland Mwaffisi
ALIYEKUWA Mbunge wa Njombe Magharibi, Yono Kevela, amesema mahasimu wake kisiasa wanatumia njia mbalimbali za kummaliza kisiasa na kutaka kumgombanisha na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula.
Kevela ameyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akikanusha habari iliyoandikwa na gazeti moja (sio Majira), lililochapisha habari yenye kichwa cha habari kinachosema “Mangula azushiwa jambo”.
Gazeti hilo lilidai Kevela anamtuhumu Mangula kwa kuvuruga uchaguzi wa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Wilaya ya Wanging'ombe kwa kuwabeba baadhi ya wagombea katika uchaguzi uliofanyika Julai 29 mwaka huu.
Habari hiyo iliongeza kuwa, siku ya uchaguzi, Mangula
akiwa amekaa meza kuu, baada ya kupewa nafasi ya kuhutubia, aliwaambia wajumbe wahakikishe, Kevela na mgombea mwingine (Nurdin), hawapiti.
“Binafsi namuheshimu sana Mangula, sijawahi kumzushia jambo lolote, yeye ni kiongozi mwadilifu, mchapa kazi na mkweli hivyo huko aliko, naomba asiwe na mtazamo hasi dhidi yangu.
“Naamini kwa maneno haya ni viongozi wangu wa chama kitaifa watnielewa, CCM inamtegemea, Mangula kwa mambo mengi
ya msingi aliyoanza kuyafanya na mafanikio yanaonekana,” alisema, Kevela.
Alisema habari iliyoandikwa na gazeti hilo haina ukweli wowote na hajawahi kuzitoa wala kuzungumza na mwandishi hivyo analitaka gazeti hilo, likanushe habari hiyo ndani ya siku 14 kuanzia leo vinginevyo atachukua hatua za kisheria.
“Sijui huyu mwandishi alipata wapi taarifa hizi, mimi najua taratibu za kushughulikia malalamiko ndani ya chama chetu, siwezi kwenda katika vyombo vya habari kwani tuna vikao vya chama ambavyo viko makini makini sana,” alisema.
Alisema yeye ni kiongozi ndani ya chama na S ambapo kichama ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa kupitia Wazazi ambapo CCM ina imani kubwa ya yeye hivyo hana tuhuma zozote katika chama wala Serikali bali ni mwanachama mwadilifu anajitolea kwa hali na mali kukitetea chama chake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment