04 December 2012

Wizara yaombwa kufunga mitandao ya picha za ngono


Na Grace Ndossa

WIZARA ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, imeombwa kutoa agizo la kufunga mitandao ya picha za ngono ili kudhibiti kasi ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI nchini.

Mwenyekiti wa asasi isiyokuwa ya kiserikali ya Better Word Organization (BWO), inayotoa elimu kwa wanafunzi, Bw. Zangina Zangina, aliyasema hayo Dar es Salaam mjana wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Alisema Wizara hiyo inapaswa kuipiga marufuku mitandao inayoonesha picha za ngono ili kupunguza maambukizi ya
virusi vya VVU kwani vijana wengi wana utamaduni wa
kuziangalia na kwenda kufanya majaribio.

“Upo umuhimu wa Wizara kuifunga mitandao ya picha za ngono
ili watu wasipate nafasi ya kuiangalia kwani inachochea vijana wadogo walio shuleni kujihusisha na mapenzi katika umri mdogo
na kupata maambukizi ya VVU,” alisema Bw. Zangina.

Hata hivyo, Bw. Zangina asasi hiyo pia inahusika kukamata CD za ngono ambazo zinasambazwa sehemu mbalimbali kwa kushikiriana na Jeshi la Polisi ili waweze kudhibiti wimbi la usambazaji huo.

Alisema kutokana na ushirikiano wanaoupata kutoka Jeshi la Polisi, hivi sasa wanazunguka maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam, kukamata CD hizo.

Hivi sasa asasi hiyo inatoa elimu katika shule za msingi na sekondari na kuwaelezea wanafunzi hatua za kuchukua ili kujikinga na UKIMWI, kuachana na vitendo viovu katika umri mdogo.

No comments:

Post a Comment