17 December 2012

Wazazi wakumbushwa kuwafunda watoto wao

 Na Neema Malley

MKURUGENZI wa kikundi cha matumaini 0nesmo John amewataka amewataka wazazi kutoa elimu juu ya ukuaji kwani ukosefu wa elimu hiyo ndio cha kinacho sababisha kuingia kwenye vishawishi hali inayopelekea kupata magonjwa ya zinaa.

Hayo yalisemwa jijini Dar es Salaam hivi karibuni alipokuwa kwenye semina ya uelimishaji lika iliyofanyika sinza ambapo ilikuwa na lengo la kutoa elimu juu ya mambo ya afya ya uzazi.

Aidha mkurugenzi huyo aliziomba serikali za mitaa zitafute njia pamoja na sera zitakazosaidia kufikisha elimu kwa vijana ili kusaidia waachane na vitendo hatarishi vinavyo wapelekekea  kupata maambukizo ya magonjwa ya zinaa.

"Tunatakiwa kupiga vita biashara haramu ya kuuza mwili inayofanywa na mabinti zetu kwani ni hatari licha ya hivyo inaenda kinyume na maadili yetu watanzania ikiwa ni pamoja kukemea mavazi yasiyo na heshima kwani ndio yanayo chochea vitendo hivyo"alisema John

Alisema kuwa tatizo la wazazi kutokaa na watoto wao na kuwapa elimu ya ukuaji kwa kuhofia kuwakuza hiyo huwa sababishia vijana kupotea ambapo huingia katika vishawishi ambavyo husabishwa na tamaa pamoja na umaskini.

Pia alitaja changamoto nyingine inayowakabili vijana ni utumiaji wa madawa ya kulevya ikiwemo uvutaji wa bangi ambayo inasababishwa na makundi rika hivyo wazazi wajitahidi kuelimisha watoto wao ili kuwaepusha na changamoto hiyo.

No comments:

Post a Comment