17 December 2012

Polisi yawasukia mkakati wanaonyanyasa wanawake





Na Moses Mabula Uyui









JESHI  la Polisi limewaonya wanaume wanaopiga wake
na watoto wao kuwa litawachukulia hatua kali ikiwa ni pamoja na kuwafikisha
mahakamani kwa kosa la kufanya ukatili wa kijinsia na watoto.



Kimweli ameitaka Jamii
kufichua na kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi vitendo vya unyanyasaji wa
kijinsia dhidi ya wanawake na watoto unaofanywa na baadhi ya watu maeneo
mbalimbali wilayani Uyui



Kauri imetolewa mkaguzi
msadizi wa polisi wa wilaya ya Uyui  Inspector
Kimweli, wakati akitoa mada katika mdahalo wa Kuhamasisha jamii juu ya
Maendeleo na usawa  wa kijinsia uliofanyika
katika kijiji cha Ilolangulu wilaya ya Uyui mkoani Tabora.



Bw. Kimweli amesema kwamba
mara nyingi wanawake pamoja na watoto wao, wamekuwa wakinyanyanswa na wanaume
kwa sababu ambazo zisizo na msingi wowote.



Kufutia hali hiyo amewataka
wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi kwa kufichua vitendo hivyo vya
ukatili ili polisi iweze kuwashughulikia watu wa aina hiyo ipasavyo, kwa
kuchakulia sheria kali ikiwa nipamoja na kuwafikisha Mahakamani.



Amesema kuwa licha ya
wanaharakati na vyombo vya dola kupiga kelele na kupinga ukatili dhidi ya
wanawake na watoto hapa nchini, bado tatizo hilo
linaendelea kuwepo na kuonya kwamba mtu atakaye kamatwa kwa kosa kama hilo hatua za
haraka za
kumpeleka mahakamani zitachukuliwa dhidi yake.



Aidha ameshauri kuwa kunzia
sasa mwanamke au mwanamme atakaye fanyiwa ukatili wa aina yoyote ile na
mwenzake asisite kutoa taarifa hizo kwa deawati la Polisi jamii katika kituo
kikuu cha mjini Tabora.



Awali mwezeshaji wa mdahalo
huo kutoka Tabora NGOs Cluster  Bw.
Cuthbert Ndogoma ameeleza kwamba lengo kuu la mdahalo, ni kutoa elimu kwa jamii
kuhusu masuala ya maendeleo na usawa kwa jamii, na kuwa mdahalo huo
umefadhiriwa na The Foundation for Civil Society.



Bw. Ndogoma amesema kwamba
Tabora NGOs Cluster kwa kushirikiana na Foundation for Civil Society, baada ya
kubaini kuwepo kwa ukatili dhidi ya wanawake na watoto unaofanywa na wanaume.


No comments:

Post a Comment