20 December 2012

Watanzania kujifunza lugha Ujerumani


Na Agnes Mwaijega

TAASISI ya Utamaduni wa Ujerumani nchini ya Geothe Institut imesema ina mpango wa kuanza kuwapeleka Watanzania wanaojifunza ya lugha ya KIjerumani kwenda Ujerumani, ili waweze kujifunza lugha hiyo zaidi.

Mkuu wa Idara ya Lugha katika taasisi hiyo Samuel Gogomoka alisema hayo Dar es Salaam jana katika sherehe za kuwakabidhi vyeti wanafunzi wa shule za sekondari za Zanaki na Chang'ombe waliofaulu mtihani wa Kijerumani.

Alisema hivi sasa Watanzania hasa wanafunzi wa sekondari wamawekuwa na mwamko mkubwa wa kusoma Kijerumani tofauti na wakati taasisi hiyo inaanza kufanya kazi nchini.

"Wakati tunaanza tulikuwa na wanafunzi wachache ,lakini hivi sasa Watanzania wana mwamko,tuna zaidi ya wanafunzi 250 sasa hivi wanaosoma Kijerumani huku 15 wakiwa siyo wanafunzi wa shule za sekondari," alisema.

Aliongeza kuwa taasisi hiyo imekuwa ikiwapeleka wanafunzi wawili Ujerumani kila mwaka kujifunza ili kuwahamasisha wengine kusoma kijerumani.

Aliwataka Watanzania kujitokeza kujifunza Kijerumani kwa sababu upo umuhimu mkubwa wa kujifunza lugha tofauti ili kufahamu lugha mbalimbali na kufanyakazi katika ofisi ambapo taasisi hiyo inatarajia kuanza kuwapeleka wanafunzi waliofaulu kwenda Ujerumani kwa gharama zao.

No comments:

Post a Comment