21 December 2012
Wafanyakazi sekta ya afya watakiwa kuwa waadilifu
Na Grace Ndossa
WAFANYAKAZI wa sekta ya afya wametakiwa kufanya kazi kwa uadilifu na kubaini wote wanaotumia au kufanya udanganyifu katika vitambulisho vya matibabu ili kusaidia Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF),kuondokana na gharama zisizo za lazima.
Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaan jana na Mama Salma Kikwete wakati akizindua huduma ya afya kwa vikundi 22vya ujasirimali vilivyojiunga na mfuko huo katika mkoa wa Dar es Salaam.
Alisema kumekuwa na malalamiko ya mara kwa mara kwa wagonjwa wanaoenda kupatiwa matibabu kwa kadi za NHIF wanaonekana wanapata huduma bure.
"Viongozi wanaosimamia sekta ya afya wanatakiwa kuchukua hatua kwa mtoa huduma yeyote atakayebainika kudharau wagonjwa wanatibiwa kwa kadi,"alisema Mama Salma.
Alisema kuwa huduma za matibabu kwa sasa ndio mtindo wa kisasa katika nchi nyingine duniani na ni wajibu wa kila mtendaji kusimamia na kutekelezwa kwa ufanisi.
Pia aliwataka kuwa walinzi wa huduma za matibabu hasa wanapokutana na lugha zisizofaa au wanapoona dawa zinazotolewa na serikali zinauzwa katika maduka ya watu binafsi watoe taarifa ili wahusika wachukuliwe hatua stahili.
Naye Waziri wa Afya Dkt.Hussen Mwinyi alisema Serikali imedhamiria kuaanda mpango mkakati wa kuchangia afya ili kila mmoja aweze kupatia matibabu kutokana na watu wengine hawawezi kulipia huduma za afya .
Dkt.Mwinyi alisema kwa sasa wana mpango wa kutoa matibabu kwa kadi(TIKA)ambayo kila mmoja atakuwa anachangia kwa kiasi fulani kitakachomsaidia kupata matibabu bure.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment