21 December 2012

SSRA yatoa mafunzo kwa wadau wa mifuko



Na Heri Shaaban

MAMLAKA ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii Tanzania (SSRA)imetoa mafunzo kwa wadau wa mifuko  kuhusiana na miongozo ya namna ya kujisajili wanachama katika mifuko ya jamii


Mafunzo hayo yalifanyika Dar es Salaam jana,na kushirikisha  wafanyakazi wa mamlaka na wadau kutoka vyama mbalimbali vya wafanyakazi

Akizungumza katika mafunzo hayo Mkurugenzi wa Sheria  wa SSRA Ngabo Ibrahimu alisema kuwa madhumuni ya mafunzo hayo kuwataka wanachama wapya wachague mifuko gani ya kujiunga.

Pia wajili wasiwalazimishe wafanyakazi katika mifuko waipendayo kwa  maslai yao binasfi kwani jukumu la kujiunga analo mfanyakazi mwenyewe.

"SSRA imetoa mafunzo  yenye lengo la kuwapanua wafanyakazi kielimu ili wasipelekeshwe na wajiri wao wakawapangia mifuko ya hifadhi ya jamii ya kujiunga wakati sio jukumu la mwajili"alisema Ibrahimu.


Aliwataka wafanyakazi wawe huru kwa kuangalia maslai yao wasibughuziwe na wajiri wao kwani jukumu la kujiunga katika mifuko ya hifadhi ya jamii analo mfanyakazi sio mwajiri.


Pia aliwataka wajili watoe fursa katika mifuko yote ili wafanyakazi wachague mifuko waipendayo kwa maslai yao wenyewe.

Kwa upande wake Katibu Mkuu  Msaidizi wa Chama cha Wafanyakazi  (TUICO)Bw.Jones Majura walipendekeza wafanyakazi wanapoachishwa kazi wawe  na malipo yatakayoweza kumpatia fedha za kula na familia kabla kupata kibarua kingine.
.
Mapendekezo hayo walipendekeza kufuatia wafanyakazi wengi baada mikataba yao ya kazi  kumalizika wanasota nyumbani bila kibarua wala mshahara huku familia zikiwategemea.

Walipongeza SSRA kwa utoaji wa mafunzo hayo kwa ajili ya utoaji wa elimu hiyo iweze kutumiwa na wafanyakazi wote nchini.

No comments:

Post a Comment