17 December 2012

Waathirika wa mabomu Mbagala wamlilia Rais

Na David John.

WAATHIRIKA wa mabomu Mbagala wamemlilia Rais Kikwete kusimamia malipo ya fidia zao ambazo mbaka sasa wengi wao bado hawajapatiwa hali inayosababisha wananchi hao kuishi maisha ya mashaka kutokana na kukosa makzi ya kudumu kama awali.


Wananchi hao wamedai kuwa wamefikia hatua hiyo baada ya Mamlaka zinazoshughulikia tatizo lao kushindwa kufanya kile ambacho kingekuwa matarajio ya wengi .badala yake wanaambilia maumivu yanayotokana na fidia wanazopewa.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam jana Mwenyekiti wa Kamati ya ufuatiliaji wa malipo hayo Steven Gimonge alisema ni vema Rais Kikwete alishughulikie sula hilo mwenyewe kuliko ilivyo sasa.

Alisema Si kwamba hundi za fedha hazitoki bali kile kinachotoka haki lingani na asala ambazo wamezipata kutokana na milipuko hiyo ya mabomu.


"Tunaamini Serikali imetoa fedha za kutosha kwa ajili ya malipo yetu lakini viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia suala hili wanatufanyia kitu ambacho si cha kawaida.alisema

Aliongeza kuwa haiwezikani mtu nyumba imebomoka kabisa alafu analipwa fidia ya Sh.2500 hadi 8000,kitu ambacho kinasikitisha na kinakatisha tamaa, hivyo bora Rais Kikwete aende akajionee hali halisi na watakuwa tayari kuonyesha hundi za malipo hayo alafu ataringanisha na uhalibifu iliojitokeza.


Naye Kimwaga Simpoi mkazi wa eneo hilo aliyekutana na janga hilo la mabomu alisema anakabiliwa na matatizo ya kiafya katika mwili wake ,na cha kusikitisha zaidi hajalipwa fidia  hadi leo.

Alisema miongoni mwa magonjwa ambayo yanamsumbua kutokana na  milipuko hiyo ni Henia,Macho kutokuona ,na kikubwa zaidi anasumbuliwa na matatizo ya kibofu cha mkojo ambacho kinatoa mikojo kila wakati.

Alisema kuwa ukweli watu wanaweza kuona kama wao wanaongopa lakini kikubwa ni kwamba kufutia tukio lile makundi mengi ya wanayodai fidia hizo yalijitokeza,ambapo wengine wamefungua hadi kesi Mahakani, lakini wao wanataka Kikwete aende Mwenyewe akaone matatizo wanayopata wananchi wake.

Tangu kutokea kwa  mabomu 2009 katika eneo la mbagala Wilayani Temeke Dar es salaam zaidi watu 300 wamejikuta wakiishi maisha ya mashaka baada ya makazi yao kuharibika na mabomu hayo, lakini mbaya zaidi Serikali bado haijalipa fidia kwa baadhi ya wananchi hao hatua ambayo inalalamikiwa vikali.

No comments:

Post a Comment