10 December 2012

Vimini sasa marufuku vyuo vya KKKT



Na Yusuph Mussa, Lushoto

MAKAMU Mkuu wa Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira kilichopo jijini Arusha, Profesa Joseph Parsalaw, amesema kuqanzia sasa ni marukufu kwa wanawake wanaosoma katika vyuo vikuu vyote na vile vishiriki vinavyomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), kuvaa suruali za kubana au vimini.


Prof. Parsalaw aliyasema hayo juzi katika mahafali ya tatu ya
Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (SEKOMU), kilichopo Wilaya ya Lushoto, mkoani Tanga na kusisitiza kuwa, lengo ni kutoa wahitimu ambao watakubalika kwenye jamii kwa matendo yao pamoja na uvaaji wao.

“Chuo Kikuu cha Tumaini kipo mstari wa mbele kuwahimiza wanafunzi na wafanyakazi kuzingatia maadili yanayokubalika kwenye jamii ya Kitanzania.

“Hivi sasa katika vyuo vyote vishiriki, tumeweka bayana aina ya mavazi ambayo yanastahili kuvaliwa na vijana ili kudumisha heshima na maadili mema,” alisema Prof. Parsalaw.

Naye Makamu Mkuu wa Chuo cha SEKOMU, Mchungaji Dkt. Anneth Munga, alisema chuo hicho ambacho pia kinatoa elimu maalumu, kitaendelea kuongeza mahitaji ya jamii.

Aliwataka wanataaluma ambao ni wahitimu katika mahafali hayo, kuwa mabalozi wazuri katika maeneo ya kazi ili jamii ijiridhishe kama wametoka katika chuo cha kanisa, kupata upako wa Mungu,
kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa na kuwanyenyekea watu.

Dkt. Munga aliwataka wasomi hao kukitangaza chuo hicho kwa mema, kuwa na moyo wa kuwakumbuka waliowashika mkono
kwa mara ya kwanza, kupata mwanga wa maisha na kuweza kuonekana mbele ya jamii.

9 comments:

  1. Hongereni kwa kuzingatia maadili ila chonde chonde isije kuwa mtaingilia mavazi ya wanafunzi wa imani nyingine. Tumeona huko France na Switzerland raia wakikatazwa kuvaa mavazi yaendayo na imani yao!

    ReplyDelete
  2. Washoneshee uniform ili mridhike na mavazi mnayoyataka wayavae.

    ReplyDelete
  3. SEKOMU kama Chuo Kikuu cha Kanisa wameanza kuonesha mfano unaotakiwa kuigwa na Vyuo vingine vyote nchini, hata vile vya Umma. Haiingii akilini kwamba kijana aliyepata elimu ya juu ndiyo anayekuwa mstari wa mbele kuvaa nguo zisizo na staha!!! Hivi wewe Dada unavaa nguo zinzoonesha maungo yako, zinabana, fupi na zinazoacha sehemu ya mwili wako uchi unajisikia vipi unapopita mbele ya watu waliokuzidi umri na wa jinsia tofauti na wewe??! Hizo nguo za namna hiyo hazikupendezi kabisa! unoanekana kichekesho tu! Ndiyo maana watu wengine hawataki hata kuongozana na wewe! Unaonekana kama kahaba fulani hivi. Acha tabia hiyo. Wazazi wako wamekupeleka Chuoni ili uelimike na uige vinavyotakiwa na siyo kuvaa nguo zinazobana!

    ReplyDelete
  4. Vyuo kazi yake ni kutoa ELIMU na siyo kutunga sheria ya jinsi mwanafunzi anavyobidi kuvaa.Nchi yetu siyo nchi inayotawaliwa KIDINI.Wanaume hao hao, hata kama wasichana watavaa buibui, ndiyo wadhambi wakubwa wa kuwaweka wasichana kama "nyumba ndogo". Tuacheni Ubinafsi.

    ReplyDelete
  5. WAKALA WA MALEZI YA VIJANA WAKO WENGI AMBAO WALIZEMBEA NA KUTUFIKISHA HAPA TULIPO NIKITAJA WACHACHE ;FAMILIA; TAASISI ZA ELIMU ;TAASISI ZA DINI ;VYOMBO VYA HABARI ;MAKUNDIRIKA NA SERIKALI WOTE WALIJIKITA ZAIDI KUSHUGHULIKIA SIASA MALEZI YA VIJANA HAKUNA ALIYEKUWA NA WAKATI UTANDAWAZI UKAMZAA MTOTO AITWAYE UTANDAZUZU ,SASA HIVI ANA MJUKUU AITWAYE UTANDAWIZI

    ReplyDelete
  6. kimini ndio kinaosoma nini nyie kueni na akiri

    ReplyDelete
  7. WEKE BASI UNIFORM BASI, SHATI JEUPE NA KHAKI KAMA MSINGI NA SEKONDARI ,HAPO MTAKUWA MMENENA KILIVYO.
    VYUO NI PERFOMANCE SIO MAVAZI.

    ReplyDelete
  8. Walimu wengi wa Vyuo Vikuu vyetu ni watupu ile mbaya. Utashangaa U-Prof wanaupata wapi. Kazi yao kuhudhulia mikutano nje ya nchi.Wanafuta allowance tu. Ukiuliza alichokifuta nini huko, anaanza kuongea "kiingereza", lugha ambayo wengi wao ni hoi hoi. Sasa wanaanza kuonea wasichana na "vimini". Basi watupe vipimo vya hivyo vimini, visivyoruhusiwa. Siketi iwe cm. ngapi toka magotini?? UJINGA MTUPU.

    ReplyDelete