21 December 2012

Uwanja wa ndege wa Mugumu wapatiwa bilioni 4.7


Na Mwandishi wetu

JUMUIYA ya Grumeti na Mfuko wa Hifadhi ya Wanyamapori wamekubali kutenga fedha kwa ajili ya mradi wa uwanja wa ndege wa Mugumu kiasi cha sh. 4.7 katika maboresho ya nyenzo zilizopo katika uwanja huo.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa Dar es Salaam jana iliyosainiwa na meneja mawasiliano wa jumuiya hiyo Shabaan Madanga, alisema uwanja huo uliopo nje ya Hifadhi ya Taifa Serengeti utakarabatiwa na kufunguliwa tena kama uwanja wa mkoa na kimataifa, ikiwa na ofisi za uhamiaji, ili kuwezesha wageni kufika kirahisi kwenye vivutio vya kipekee vya wanyamapori.

Taarifa ilieleza kuwa mpango wa uwanja wa ndege Mugumu umekwisha kubaliwa na Serikali ya Tanzania pamoja na mashirika mengine yanayohifadhi mazingira kama Mamlaka za Hifadhi za Taifa (TANAPA)

Uwanja huu wa kimataifa wa Mugumu, unajengwa nje ya Hifadhi ya Taifa Serengeti, kwenye eneo la mbali mkoani Mara, ambalo liko nyuma kiuchumi.

Uwanja huu hautashindana na viwanja vikubwa vya kimataifa kama Kilimanjaro na Mwanza, ila utawezesha Magharibi ya Serengeti kufikiwa kirahisi na ndege ndogo pamoja na za kati aina ya Turboprop, kama vile Twin Otter na Cessna ambazo tayari hutumika kwa ajili ya safari za ndege kwenda Serengeti.

Hivi sasa, waendeshaji wa makampuni ya safari za kitalii hutumia Kiwanja cha ndege Seronera ambacho kiko katika kitovu cha Hifadhi ya Taifa Serengeti.Mugumu iko nje ya Serengeti kwa hiyo ni njia mbadala ya utalii endelevu usioathiri mazingira.

"Uwekezaji katika miundombinu ya ndani utaleta faida kubwa kiuchumi kwa jamii zenye hali duni kimaisha pembezoni mwa Magharibi mwa Serengeti, kwa kuzalisha ajira na kuzalisha mapato ikiwa ni matokeo ya ongezeko la shughuli za kitalii,".

No comments:

Post a Comment