21 December 2012

Matukio ya dawa za kulevya yaongezeka- Polisi


Zena Mohamed na Neema Malley

JESHI la Polisi nchini limesema kiwango cha ukamataji wa wahalifu wa matukio ya dawa za kulevya umeongezeka kwa kiasi kikubwa nchini ikilinganishwa na mwaka jana.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Naibu Kamishina wa Polisi wa Makosa ya Jinai nchini, Issaya Mngulu alisema uhalifu kwa kipindi cha mwezi Januari hadi Novemba mwaka huu
kilo 55499 za dawa hizo na wahalifu 6933 walikamatwa ukilinganisha na mwaka jana ambapo zilikamatwa kilo 17776 na watuhumiwa 211.

Alisema kwa katika kipindi hicho matishio mengi ya usalama yalijitokeza licha ya Jeshi la Polisi kukabiliana nayo ni pamoja na ugaidi,uharamia baharini,uhamiaji haramu na biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu.

Matishio mengine ni Tatizo la uharifu dhidi ya mazingira na maliasili,uingizwaji wa bidhaa bandia,uingizwaji wa silaha haramu,dawa za kulevya,migogoro ya kisiasa,kidini pam oja na migogoro ya wanafunzi wa taasisi na vyuo vya  elimu ya juu ambapo matukio hayo ylisababisha vifo,majeruhi na uharibifu wa mali.

Alisema hali ya uharifu nchini inapimwa kwa kulinganisha makosa yaliyotolewa taarifa katika vituo vya polisi kwa mwaka hadi mwaka ambapo makosa ya jinai yaliyotolewa taarifa katika vituo vya polisi mwaka huu ni 66255 ikilinganishwa na makosa 69678 katika mwaka 2011 ni sawa na upungufu wa asilimia 4.9.

"Mchanganuo wa takwimu hizi ni kielelezo dhahiri kuwa kumekuwepo na upungufu wa kuridhisha wa makosa makubwa ya jinai hapa nchini ambapo sababu kubwa ni ushirikiano kati ya jeshi la polisi na wananchi katika kutoa taarifa",alisema Mngulu.

Pamoja na hayo Mngulu alisema jeshi hilo limejiwekea mikakati mbalimbali ili kuzuia na kukabiliana na uhalifu ikiwemo kutambua maeneo nyeti yenye vivutio vya uhalifu na kuyapangia ulinzi,misako na doria imara.

Pia alitoa wito kwa taasisi mbalimbali za serikali,asasi za kiraia,sekta binafsi za ulinzi,vyama vya siasa,madhehebu ya dini na wananchi kwa ujmla katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka kila mmoja kuendelea kutoo ushirikiano kwa jeshi la polisi na kutoa taarifa zitakazo wezesha kukabiriana na uhalifu na wahalifu kote nchini.

No comments:

Post a Comment