21 December 2012

RC Dar aziagiza Manispaa kutekeleza miradi


Na Heri Shaaban

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Meck Sadiki, ameziagiza Manispaa za Mkoa huo kutekeleza miradi ya maendeleo ambayo hadi mwishoni mwa Julai na Septemba mwaka huu, kiwango cha utekelezaji wake kilikuwa chini sana.


Bw. Sadiki alitoa agizo hilo Dar es Salaam juzi katika Kikao cha Kamati ya Ushauri Mkoa (RCC), ambacho baadhi ya washiriki
wake ni wabunge wa Mkoa huo na Wakurugenzi.

Alisema Manispaa za Temeke, Ilala na Kinondoni zimeshindwa kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo mwaka huu bila sababu za msingi hivyo kukwamisha maendeleo ya wananchi.

“Walipa kodi wakubwa ni wananchi ambao fedha zao ndio zinazofanikisha miradi husika pamoja na vyanzo vya mapato
katika manispaa ambavyo vinapaswa kutumika vizuri.

“Miradi yote ya maendeleo inatekelezwa kwa kuzingatia ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), manispaa zote tatu zihakikishe wafanyabiashara wanaopanga bidhaa zao katika maeneo ambayo hayaruhusiwi kisheria (barabarani), wanaondolewa pamoja na
magari yanayopaki maeneo ambayo si rasmi,” alisema.

Awali Bw. Sadiki alitoa agizo hilo lakini watendaji wa manispaa hizo wameshindwa kulitekeleza kwa kiwango cha kuridhisha.


No comments:

Post a Comment