13 December 2012
TRL waanza kufanyia kazi agizo la Waziri
Na Rose Itono
UONGOZI wa Shirika la Reli nchini (TRL), umelipokea agizo
la Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Charles Tizeba, aliyetaka wafanyakazi wawili wa shirika hilo wanaodaiwa kutafuna nauli
za abiria na mizigo, wafukuzwe kazi mara moja.
Kauli hiyo ya ilitolewa Dar es Salaam jana na Ofisi ya Uhusiano TRL kwa niaba ya Mkururgenzi Mtendaji, Mhandisi Kipallo Kisamfu, wakati gazeti hili lilipotaka kujua hatu ambazo shirika limechukua juu ya watumishi hao kama alivyoagiza Dkt. Tizeba.
“Agizo hili tunalifanyika kazi kulingana na taratibu za kikazi, kwa vile ni mchakato wa kinidhamu tahadhari zote zitachukuliwa kuona agizo hilo linatekelezwa vizuri kulingana na kanuni na taratibu za kinadhamu zinazotawala ndani ya TRL,” alisema.
Alifafanua kuwa, TRL ina utaratibu wake unaozingatia nidhamu
na uwajibikaji kazini, hivyo kila mtumishi ambaye huthibitika kujihusisha na vitendo vya aina hiyo, kuzembea kazi na kusababisha hasara kwa kampuni, mtuhumiwa hupewa taarifa rasmi ya kujileza na hatimaye ikionekana kuna haja ya kumfikisha katika mamlaka za kinidhamu kulingana na ngazi yake hatua hiyo huchukuliwa mara moja.
Alisema hatua hiyo hufikiwa baada ya majadiliano na uchambuzi wa pande mbili yaani mashitaka na utetezi.
“Mara nyingine kama kosa ni la kijinai, mtuhumiwa hufikishwa katika vyombo vya dola kwa hatua husika,” alisema na kuongeza kuwa, michakato ya kuwaadhibu watumishi wanaokiuka maadili na taratibu za kazi ni endelevu na haisubiri matamko ya viongozi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment