18 December 2012
Terezya 'awasuta' viongozi *Akasirishwa na uchafu wa mazingira
Na David John
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dkt. Terezya Huvisa, amewashukia viongozi wa Manispaa ya Jiji la
Dar es Salaam na wadau wa mazingira kwa kushindwa kuliweka
jiji hilo katika hali ya usafi mbali na kupokea fedha nyingi kutoka kwa wadau wa mazingira duniani.
Aliwataka viongozi hao kumweleza kama wameshindwa kazi ili afikishe taarifa kwa Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal, ili aweze kuchukua hatua zaidi.
Dkt. Huvisa aliyasema hayo Dar es salaam jana wakati wakati akizindua taalifa ya hali ya mazingira jijini humo na kusisitiza
kuwa, anashangaa kuona nchi kama Rwanda na Msumbiji
zimechelewa kupata uhuru wake nyuma ya Tanzania lakini
zinafanya vizuri katika usafi wa mazingira.
“Nchi kama Msumbiji na Rwanda, zimepiga hatua kubwa katika eneo la mazingira, kila kiongozi aliyepo katika eneo hilo anafanya kazi kwa bidii na kujituma wakisimamia sheria zilipo lakini hapa kwetu kama hakuna viongozi ambao wamepewa dhamana, kama mmeshindwa kazi semeni tuchukue hatua,” alisema.
Alisema awali Dkt. Bilal alizindua kampeni ya usafi katika manispaa zote za jiji hilo lakini inashangaza manispaa moja pekee ya Ilala ndio inayofanya kazi vizuri na nyingine zimekithiri kwa uchafu.
“Nawapongeza watu wa Ilala, mmejitahidi kusimamia suala zima
la mazingira lakini Manispaa za Temeke, Kinondoni aibu tupu cha kusikitisha zaidi, malipo yanaonekana kufanyika katika magari ya kuzoa taka lakini mazingira bado machafu hizo pesa zinakwenda wapi,” alihoji Dkt. Huvisa.
Aliongeza kuwa, amefanya ziara ya kushutukiza katika maeneo ya Kinondoni na kutoa maagizo lakini hali ya uchafu bado imekithiri katika Wilaya hiyo pamoja na Temeke.
Alisema hali hiyo ni aibu katika nchi hasa ukizingatia kuwa, Jiji la Dar es Salaam linapaswa kuwa safi muda wote na mfano wa kuigwa dhidi ya mikoa mingine nchini.
Akizungumzia taarifa hiyo, Dkt. Huvisa alisema uhai wa jamii unategemea rasilimali za mazingira ambapo hifadhi ya mazingira inakumbana na changamoto nyingi.
“Lipo tatizo la wananchi wengi kuhamia mijini hivyo kusababisha ongezeko la changamoto za uharibifu wa mzingira, watu wanapoongezeka ni weazi taka zinakuwa nyingi, uchafu wa
maji na hewa, upeteaji wa bioanuai, uharibifu wa vyanzo
vya maji na miundombinu,” alisema.
Aliongeza kuwa, chagamoto hizo zinaenda sambamba na madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi hivyo umakini unahitajika katika udhibiti ili kuwa na matumizi endelevu ya rasilimali kwa maendeleo endelevu.
Dkt. Huvisa alisema katika mkutano wa tisa Mawaziri wa Afrika (AMCEN), uliofanyika mjini Kampala, nchini Uganda Julai mwaka huu, ulibainisha ukosefu wa taarifa za hali ya mazingira katika Bara la Afrika kama moja ya sababu zinazochangia mipango duni ya usimamizi wa shughuli za maendeleo na utekelezaji wa
mikataba ya utunzaji mazingira.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment