18 December 2012

TBS kukutana na wazalishaji sabuni



Na Peter Mwenda

WADAU wanaozalisha sabuni na dawa za kuondoa uchafu, wanatarajia kukutana Desemba 17-19 mwaka huu, kujadiliana mapendekezo ya kuimarisha umoja wao katika Soko la Afrika Mashariki.


Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Shirika la Viwango nchini (TBS), Bw. Leandri Kinabo, alisema mkutano huo utajadili mapendekezo 14.

“Lengo la mkutano huu ni kujadili umoja na mshikamano wao ili kuboresha bidhaa za sabuni na dawa za kuondoa uchafu katika Soko la Afrika Mashariki,” alisema Bw. Kinabo.

Alisema mapendekezo ya jumla ambayo yatafikiwa katika mkutano huo yatawasilishwa kwenye mkutano wa Afrika Mashariki ambao umepangwa kufanyika Januari 7-11 mwakani, jijini Dar es Salaam.

Aliongeza kuwa, hivi sasa wadau wanaotengeneza sabuni na dawa za kuondoa uchafu katika kipindi hiki cha utandawazi, wanapaswa kuboresha bidhaa zao ili ziweze kuwa na kiwango katika soko.

Bw. Kinabo aliwaomba wadau husika wajitokeze kwa wingi katika mkutano huo ili kujua nafasi ya bidhaa zao kwenye Soko la Afrika Mashariki.

No comments:

Post a Comment