21 December 2012
Propaganda za wanasiasa zazua jambo mkoani Mara
Na Raphael Okello,Musoma.
WAKAZI wa Musoma mkoani Mara wamekerwa na tabia ya wananchi wengi kupendelea propaganada ya wanasiasa kuliko elimu inayotolewa na Wataalam.
Wakiwa katika mdahalo jana kuhusu mabadiliko ya tabia ya nchi mjini Musoma uliondaliwa na Jukwaa la Maendeleo mkoani Mara(MDF) kwa ufadhili wa The Foundation For Civil Society walitaka Watanzania kubadili mtazamo wa kutoipenda zaidi siasa na kupuuzia mikutano
ya wataalamu.
Akichangia hoja juu ya elimu ya mazingira,Deric Mbangu mkazi wa Kamunyonge alishangazwa na kitendo cha wananchi wengi kupenda propaganda ya wanasiasa kuliko elimu ya wataalam pia kutopendelea kusoma vitabu na majarida yanayotoa elimu.
Alisema kitendo hicho hufanya watu wengi kuishi maisha magumu kwa kupuuza kupata habari za kitaalamu ikiwa ni pamoja na mazingira
yao ambapo kama wangezingatia mambo ya kitaalam yangesaidia kupammbana na uchafuzi wa mazingira.
“hapa tunajadili mambo muhimu ambayo ni mazingira yanayomhusu kila mtu lakini
mahudhirio ya watu hayawezi kulinganishwa na mikutano ya wanasiasa……angekuwa ni
mwanasiasa fulani uwanja wa mkendo ule wote ungejaa watu, hii ni ajabu sana alisema
Mbangu.
Alisema katika siku za hivi karibuni,ushawishi mkubwa wa watu unaelekea zaidi kwenye siasa ambapo alipendekeza suala la mazingira liingizwe katika mtaala wa taaluma zote kwa kuwa ni suala linalowahusu wote.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment