21 December 2012
limu Mkinga waonyesha mwitikio utalii wa ndani
Na Mwandishi Wetu,Pangani
WALIMU 18 wa Shule za Msingi katika Kata za Maramba,Mapatano na Mhinduro wilayani Mkinga mkoani Tanga wameanza kuitikia wito wa Serikali unaohimiza kuwepo utalii wa ndani kwa lengo la kukuza sekta hiyo muhimu kwa maendeleo ya Taifa.
Walimu hao walitembelea hifadhi ya Taifa ya Saadan iliyoko wilaya za Pangani na Bagamoyo ambapo wamejifunza mambo mbalimbali yanayohusu hifadhi hiyo pekee inayoungana na bahari.
Akizungumza baada ya kutembelea hifadhi hiyo,Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Lugongo,Yohana Philemon alisema ziara hiyo imewaongezea uelewa wa kutosha walimu hao na kwamba itawasaidia katika uboreshaji ufundishaji masomo ya maarifa ya Jamii.
Alisema ziara hiyo imeratibiwa na Saida Ramadhani,Clement Shehiza ambapo wamewashukuru wahifadhi hao wa hifadhi ya Saadan kwa juhudi kubwa wanazofanya katika kuhakikisha utunzaji wa mazingira unaboresha.
Aidha walimu hao wamewataka wananchi kujenga utamaduni wa kutembelea hifadhi za Taifa kwani ni sehemu muhimu ya kuongeza uelewa na kukuza sekta ya utalii wa ndani hapa nchini.
Waliwataka walimu na jamii kwa ujumla kutenga muda maalum hasa wa mapumziko kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo jirani na makazi yao ili kukuza uelewa wa sekta hiyo muhimu kwa maendeleo ya nchi.
Alisema mpango wa kutembelea vivutio vya utalii umeanzishwa na walimu hao kwa lengo la kuongeza ufahamu ili waweze kufundisha kwa mifano sahihi masomo yanayohusiana na sekta hiyo na kuitaka Serikali kuendelea kuboresha mazingira ya walimu ili waweze kupanua wigo zaidi wa kutembelea maeneo hayo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment