18 December 2012
NRA kutoa elimu ya uraia
Na Mwandishi Wetu
CHAMA cha siasa cha National Reconstruction Alliance (NRA), kipo mbioni kutoa elimu ya uraia kwa wananchi ili waweze
waweze kujua haki zao.
Mwenyekiti wa vijana wa chama hicho katika vyuo vikuu nchini,
Bw. Bilal Sadick, alisema uamuzi huo umefikiwa kwenye kikao kilichofanyika mkoani Morogoro.
“Katika kikao hiki, tulikubaliana tuanze kutoa elimu ya uraia kwa wananchi ili waweze haki zao za kupiga kura na kuchagua chama wanachokitaka bila kushawishiwa,” alisema Bw. Sadick.
Alisema katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwaka 2010, takwimu zinaonesha kuwa, asilimia 40 ya Watanzania hawajapiga kura kwa sababu ya kukosa elimu ya uraia.
Katika hatua nyingine, Bw. Sadick alisema vijana wa vyuo vikuu wenye mapenzi na siasa pamoja na wadau wengine watafanya kongamano la kujadili Tanzania waitakayo.
Alisema kongamano hilo limepangwa kufanyika Desemba 21 mwaka huu, katika Chuo Kikuu cha Kiislamu, kilichopo mkoani Morogoro na kushirikisha viongozi mbalimbali wa matawi katika
vyuo vikuu nchini.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment