18 December 2012

Mwandishi Majira apata tuzo



Na Rachel Balama

MWANDISHI wa gazeti la Majira, Bi. Anneth Kagenda, amepata tuzo ya uandishi bora wa habari za vijijini, Wilaya ya Mkuranga, mkoani Pwani, kwa kuandika habari za mazingira, utabiri na huduma za tiba asili.


Tuzo hiyo imetolewa juzi Mkuranga na mganga wa tiba za asili
Dkt. Kassim Mswahili, ambaye alisema Bi. Kagenda, amepewa
tuzo hiyo kutokana na kuandika habari nyingi za kuelimisha
jamii na utoaji huduma ya tiba asili na utabiri wilayani humo.

Alisema mwaka 2011, alitabiri masuala mbalimbali kama ajali, mafuriko na wizi ambapo gazeti la Majira liliandika habari hizo
na badaye utabiri huo ilitimia.

“Mwandishi huyu amekuwa akifuatilia habari za Kilimahewa wilayani hapa, nilipofanya uchunguzi niligundua anastahili
kupata tuzo hii,” alisema Dkt. Mswahili.

Aliitaka jamii kuheshimu utabiri unaotolewa na wataalamu wa
tiba asili ili kujiepusha na athari zinazoweza kutokea.

Alisema tuzo hiyo ni ya kwanza kutolewa kwa mwandishi wa
habari na ataendelea kuitoa kila mwaka. Naye Bi. Kagenda
alimshukuru Dkt. Mswahili kwa kutoa tuzo hiyo.

No comments:

Post a Comment