18 December 2012
Gari lakanyaga mtoto, afariki dunia
Leah Daudi na Angelina Faustine
MTOTO Mohamedi Stamili, mwenye umri wa mwaka mmoja, amefariki dunia Dar es Salaam juzi, baada ya kukanyagwa na
gari wakati akicheza uvunguni.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Temeke, Engelbert Kiondo, alisema tukio hilo lilitokea saa 12 jioni, katika eneo la Kisota Kigamboni ambapo gari ilikuwa na namba za usajili T 972 BFT, aina ya
Nisani X-Trail, iliyokuwa ikiendeshwa na Bw. Moses Edward.
“Huyu mtoto alikuwa akicheza chini ya uvungu wa gari ambalo lilikuwa limepaki kwenye geti na dereva alipoingia ndani ya gari, aliliwasha na kumkanyanga mtoto ambaye alifariki kapo hapo.
“Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Vijibweni, dereva amekamatwa na upelelezi unaendelea,” alisema.
Katika tukio jingine, moto umezuka ghafla kwenye nyumba ya mkazi wa Tabata Machimbo, Elinestina Machael (30), ambao uliteketeza vyumba viwili na mali zote zilizokuwemo.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, Marietha Komba, alisema moto huo ulizuka juzi saa 12 jioni ambao undaiwa chanzo chake
ni hitilafu ya umeme.
Alisema thamani ya mali iliyoteketea bado haijafahamika ambapo moto huo ulizimwa na wakazi wa eneo hilo na hakuna madhara
yaliyotokea kwa binadamu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment