21 December 2012
Mtoto miaka 3 abakwa na baba yake
Na Steven William, Muheza
MTOTO mwenye umri wa miaka mitatu (jina tunalo), ameharibiwa vibaya sehemu za siri baada ya kubakwa na baba yake wa kambo aliyefahamika kwa jina la Bw. Yakob Raimon.
Tukio hilo limetokea juzi katika Kijiji cha Paramba, kilichopo
Kata ya Kicheba, Wilaya ya Muheza, mkoani Tanga.
Akizungumza na Majira katika Hospitali Teule ya Muheza, mama wa mtoto huyo Bi. Maria Renard, alisema siku ya tukio alimuacha mtoto huyo nyumbani akiwa na shangazi yake aliyemtaka kwa jina la Bi. Maria Raimondi na kwenda kanisani katika mafundisho ya kipaimara.
Alisema baada ya kuondoka, ghafla baba wa kambo wa mtoto huyo alikwenda na kumchukua akidai anakwenda kumpa dawa nyumbani kwani kwani alikuwa akisumbuliwa na homa.
“Baada ya kufika naye nyumbani kwake, alianza kumbaka ambapo mtoto alilia sana kutokana na maumivu aliyokuwa akiyapata,” alisema Bi. Renard.
Alisema baada ya shangazi huyo kuona mtoto anachelewa kurudishwa, aliamua kwenda kumfuatilia na kumkuta akitokwa
na damu nyingi sehemu za siri bila kumkuta baba yake.
“Nilipewa taarifa za tukio hili wakati nipo kanisani hivyo nilirudi nyumbani haraka na kumkuta mwanangu katika hali mbaya, nilitoa taarifa kwa uongozi wa kijiji na kumleta hapa hospitali,” alisema.
Kwa upande wake, daktari wa zamu katika wodi ya watoto hospitalini hapo (jina tunalo), alisema mtoto huyo baada ya kupimwa na daktari bingwa wa upasuaji (jina tunalo),
alionekana amebakwa na kuchubuka sehemu za siri.
Kamanda wa Polisi mkoani humo, Costantine Massawe, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kudai wanaendelea kumsaka mtuhumiwa ili aweze kufikishwa mahakamani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment