03 December 2012
Maadhimisho ya UKIMWI yaiongia dosari Na Timothy Itembe, Tarime
MAADHIMISHI ya Siku ya UKIMWI, mkoani Mara, yameingia dosari baada ya walengwa (waathirika), kushindwa kuhudhuria
kwa madai ya kutoshirikishwa.
Kimkoa maadhimisho hayo yalipangwa kufanyika katika Kijiji cha Itiryo, wilaayani Tarime, ambapo Mkuu wa Wilaya hiyo, Bw. John Henjewele, alikataa kusaini kitabu cha wageni.
Hatua hiyo ilitokana na Bw. Henjewele, kufika kijijini hapo na kukuta walengwa (waathirika), hawapo na kudai maadhimishi
hayo hayakufanyiwa maandalizi ya kutosha.
“'Nimeshangazwa kuona kuwa walengwa wa siku hii hawapo, watu waliopewa jukumu la kuratibu hawakufanya maandalizi mazuri ya kuwajali wananchi na watu waishio na virusi vya UKIMWI,” alisema Bw. Henjewele.
Katika maadhimisho hayo, idadi kubwa ya watoto ndio iliyoshiriki wakiwemo wa Shule ya Msingi Itiryo, wapiga tarumbeta pamoja na watumishi mashirika yanayotoa elimu ya ugonjwa huo ili kuzuia maambukizi mapya ya UKIMWI.
Kutokana na hali hiyo, Bw. Henjewele aliamua kutembelea na kukagua mabanda ya matangazo bila kusaini kitabu cha wageni akimwakilisha Mkuu wa Mkoa huo, Bw. John Tuppa ambaye alibanwa na shughuli nyingine za kikazi na baaadaye kuondoka.
Maandalizi ya maadhimisho hayo yaliandaliwa na Halmashauri ya Wilaya kupitia kitengo cha Idara ya Maendeleo ya Jamii ambacho ndio kinadaiwa kushindwa kuwaalika walengwa.
Mwathirika wa ugonjwa huo, Bi. Pili Alumasi, alidai pamoja na kwenda hospitali kila mara ili kuchukua dawa, hawajapewa taarifa zozote za kuhamasishwa kushiriki katika maadhimisho hayo.
“Sisi tumesikia mitaani kuwa kuna maadhimisho ya siku ya UKIMWI katika Shule ya Msingi Itiryo, Kata ya Nyamaraaga,
lakini hatukushirikishwa kwa sababu mashirika yetu ya watu
waishio na VVU yanadaiwa fedha na Halmashauri ambazo
walizikopo miaka mingi iliyopita,” alisema Bi. Alumasi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment