03 December 2012
'Katiba mpya iwalinde albino'
Na Rehema Maigala
KATIBA mpya imeombwa kutoa ulinzi na usalama kwa albino ambao wamekuwa wakikatwa viungo bila hatia yoyote na kubakia wakiwa na ulemavu.
Hayo yalisemwa Dar es Salaam juzi na Miss Tanzania wa mwaka huu,Brigitte Alfred katika viwanja vya Tanganyika packers ambapo wananchi walikuwa wakitoa maoni yao kuhusiana na maandalizi ya katiba mpya.
Alisema albino wamekuwa wakiishi bila amani japokuwa wako kwenye nchi yao na wana haki kama wengine.
Alisema hayo yote yanatokana na watu kudanganywa na waganga wa kienyeji kwamba wakipeleka viungo vya albino watapata utajiri.
Aliongeza kuwa katiba mpya itamke wazi adhabu ya mtu yeyote atakayehusika na kumsababishia ulemavu albino au kumua.
Alisisitiza kuwa katiba hiyo pia ihimize serikali kuwaangalia uwezekano wa kuwapatia ajira walemavu wote ajira ili kupunguza idadi ya ombaomba.
"Hali ya ukosefu wa ajira kwa walemavu wengi inasababisha kuongezeka kwa idadi ya ombaomba katika mitaa mbalimbali ya miji," alisema.
Pia alisema katiba mpya iwajali vijana kwa kuwapatia ajira ili waondokane na hali ya umasikini iliyokithiri miongoni mwa vijana hao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment