13 December 2012
Jela miaka 30 kwa kumbaka mwanafunzi
Na Raphael Okello, Musoma
OFISA Mtendaji wa Kijiji cha Mabui Marafuru, Bw. Benedicto Sonanga (42), amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela baada Mahakama ya Wilaya ya Musoma, mkoani Mara, kumtia hatiani kwa kosa la kumbaka mwanafunzi wa Shule ya Sekondari
Mugango mwenye umri wa miaka 16 (jina linahifadhiwa).
Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Faisal Kahamba, ambaye alisema mshtakiwa alivunja sheria ya ndoa
kwa kumshawishi na kufanya ngono na binti mwenye umri
chini ya miaka 18.
Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Kahamba alidai kitendo cha mshtakiwa kufanya ngono na binti huyo ni kusa kisheria pia
ni aibu kwa mtumishi wa Serikali aliyekabidhiwa dhamana
na wananchi kusimamia na kutekeleza sheria, kanuni na
taratibu ya nchi.
Awali Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Bw. Jonas Kaijage, alidai kuwa, mshtakiwa alitenda kosa hilo Mei 6, 2009, katika eneo la Mabui Marafuru.
Alisema mshtakiwa alirubuni binti huyo kuwa atamlipia karo ya shule na kufanya naye ngono kinyume cha sheria inayowalinda watoto.
Mshtakiwa alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Mei 21,2009 ambapo baada ya pande zote kutoa ushahidi, mahakamani ilimtia hatiani na kumuhukumu kifungo hicho gerezani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment